Tundu Lissu: Watekaji wanataka wanimalize wamsingizie Mbowe
Samia kapewa maelekezo na waarabu ya kulinda ''uwekezaji'' wao. Wametoa fedha nyingi za kuhonga vyama vya upinzani ili visimpe upinzani na kuanika uovu wake na wakati wa uchaguzi visitoe upinzani kamili. Lissu pekee ndiye aliyekataa hii hongo ndiyo maana wanapanga njama za kumuumiza. Unakumbuka yule simba wa kwenye maonyesho ambaye Samia alisema ''hatulii kama Lissu'' hivyo aitwe Lissu? Alikuwa anamaanisha hatulii hata akipewa fedha!
Duuh
 
Uchaguzi wa CDM,kijani ndio wanateseka nao hakika Lissu ni Muujiza unaotembea
Ndio maana ya hii katuni
images (1).jpeg
 
Samia kapewa maelekezo na waarabu ya kulinda ''uwekezaji'' wao. Wametoa fedha nyingi za kuhonga vyama vya upinzani ili visimpe upinzani na kuanika uovu wake na wakati wa uchaguzi visitoe upinzani kamili. Lissu pekee ndiye aliyekataa hii hongo ndiyo maana wanapanga njama za kumuumiza. Unakumbuka yule simba wa kwenye maonyesho ambaye Samia alisema ''hatulii kama Lissu'' hivyo aitwe Lissu? Alikuwa anamaanisha hatulii hata akipewa fedha!
💯%
 
Enyi watu wabaya mjulikanao kama 'watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama, Freeman Mbowe.

Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17. Na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.

Ndivyo mnavyofanya kila mnapoua watu wasio na hatia. Mnasingizia watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu.

Huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani. Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo bungeni.

Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan. Badala ya kumlinda mtamchafua zaidi. Na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia.View attachment 3178142
Duh 🙄 !
 
Kutoka X Lissu anaandika,

Enyi watu wabaya mjulikanao kama 'watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama, Freeman Mbowe.

Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17. Na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.

Ndivyo mnavyofanya kila mnapoua watu wasio na hatia. Mnasingizia watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu.

Huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani. Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo bungeni.

Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan. Badala ya kumlinda mtamchafua zaidi. Na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia.
CCM ni wauaji wakubwa, cjui mtu unakuwaje mwanachama wa hili genge!
 
Duh hawatafanikiwa na hawatafanikiwa huu ujinga waliutumia kwa chacha wangwe hawatafanikiwa kamwe

We are watching them24/7 wakijaribu tunapindua kabisa serikali na ndio utakuwa mwisho wa CCM!!
kah!
 
Back
Top Bottom