Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

kwahiyo ushenzi huo uhalalishwe mashuleni? kwani USWAZI kuna maadili? ndiyo maana kukaitwa uswahili, uncivilized society.... ni derogatory term kwa watu wa huko USWAZI...
Huyo waziri ambaye ni kilaza mwenzio
Ambaye ni sehemu ya maamuzi ya serikali
Ameshindwa kuzuia huo wimbo usiingie kwenye jamii matokeo yake anakuja kuazibu walimu ambao wanacheza wimbo ambao ni wimbo halali ambao serikali imeruhusu uwafikie wananchi ikiwemo hao watoto

Ambao wanauimba kama wameutunga wao
Kosa la mwalimu hapo ni lipi
Mbona naona kama waziri ndiyo mwenye makosa?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Duu mkuu naona wamekuvuruga, umepandwa na hasira kama umemwagiwa maji, maji ya betriii
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Walimu ni wazazi wetu na hadi tumefika hapa ni kwa nguvu ya Walimu.

Na hili kundi limekuwa likionewa sana na kutumiwa vibaya.
 
Kwani target ni nini? Mtoto awe na maadili ya kinafiki anapokuwa shuleni tu?.

Ndo maana wakikua wanakuwa na unafiki wa maadili kumbe ni majizi ya kalamu, mafisadi, mamalaya. Ni kwa sababu ya unafiki waliokuzwa nao. Mtoto anajua wimbo wote badala ya watu kujiuliza kwanini watoto wanajua verse za wimbo wote wanatafuta kiki za kisiasa.
Unataka ku establish nini? Very strange! Kuwa tusiwe wanafiki , tufanye mapenzi (sex intercourse) sebuleni kwa vile watoto wanajua kuwa baba na mama wanafanya ndiyo tukazaliwa? What are you trying to establish! take home msg ni ipi?
 
Uamuzi waliochukua sio suruhisho. Suruhu kubwa ni kufungia na kuzuia nyimbo hizo kuimbwa maana hazina maadili kabisaaaaaaaa! Mamlaka zinazohusika yaani BASATA walione hili na kuchukua hatua Kwa nyimbo ambazo hazina maadili. Msanii wakiume anavaa kanga Moja na kupanda jukwaani manaake Nini? Na wengine wengi kabisa
Maamuzi yaliyochukuliwa ni sahihi kabisa iwe fundisho kwa wakuu wote wa shule Tanzania ,kusimamia taaluma na maadili mazuri
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Wanafanya hivi kwa sababu hawana maadili na mamlaka zinazohusika hazina maadili pia.
 
Unataka ku establish nini? Very strange! Kuwa tusiwe wanafiki , tufanye mapenzi (sex intercourse) sebuleni kwa vile watoto wanajua kuwa baba na mama wanafanya ndiyo tukazaliwa? What are you trying to establish! take home msg ni ipi?
Nataka uhalali wa kumtumbua mwalimu kwa kosa la kucheza wimbo kwenye tukio moja ilihali waziri aliyeruhusu huo wimbo upigwe miezi na miezi mpaka watoto wakaukariri hana kosa na yupo ofisini.
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Ndio soko linataka hivyo, si waona hata wewe umekalili hicho kipande.
 
Watoto wanavyoimba inaonesha wanaujua wimbo tangu awali, this means kwamba kwa siku hiyo tu mwalimu mkuu hajasababisha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi.
Nakazia hapo, kama kucheza na kufuatiza huo mziki ndio kosa, basi waziri ajue wanafunzi wameyajulia hayo mashairi uraiani
 
Wakirudishiwa vyeo walivyonyang'anywa, mimi nitakwenda kufungua kesi mahahakani. Nampa hongera sana Mh. Waziri wa Elimu kwa hatua sahihi alizochukua
 
Mmh najaribu kutafakari na kuona kosa la walimu mpaka kuvuliwa nyadhifa zao sioni.

Tujiulize haya!

1.Je kosa ni kurekodiwa na kuwekwa katika social media au

2. Mziki kupigwa maeneo ya shule na watoto kucheza.

3. Je ingekuwa siku ya mahafali ya Darasa la saba na wimbo huo ukapigwa na wanafunzi wakaucheza je mwalimu angevuliwa nyadhifa yake?

Kiukweli tunakemea mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu lakini mpaka wimbo umepita basata walichuja wapi na kuona utatumika kwaajili ya wakubwa tu na watoto hawata sikiza wimbo huo?

Watoto wanavyoimba inaonesha wanaujua wimbo tangu awali, this means kwamba kwa siku hiyo tu mwalimu mkuu hajasababisha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

Kumvua cheo mwalimu mkuu ni Kuiambia BASATA kuwa walikosea kuruhusu wimbo huo.
Kwa maoni yangu mwalimu mkuu hana makosa ya kumvua cheo chake.

Yani Kiukweli mawaziri hukurupuka sana katika maamuzi, sijui ni poor kantiri ndo maana na mindset zetu zipo kama hali yetu ya uchumi.

Honeeey.
Haniiii
 
Tatizo la Malaya kuvamia muziki linaanza kuonekana. Hivi hakuna vya kuimba zaidi ya mitusi.
Huyohuyo Zuchu unayemwita Malaya
Alialikwa na hao hao mawaziri,mwezi uliopita huko Geita,
Akaenda kuimba huo huo upuuzi wa honey, na upuuzi mwingine wa kwikwikwi sijui sugar sukari,,huku akiwakatia mauno na wakamshangilia.

Kama kweli wanataka kukomesha huu upuuzi,waanze wao kujitumbua ,waachie ngazi,
Ndio waje kutumbua walimu.

Na bado anapeta tu kwenye tasnia
Hakuna kitu wamemfanya.
 
Back
Top Bottom