Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunaviongozi wavivu wenye fikra duni wanashughurika na matokeo badala ya kudeal na chanzo cha matatizo.

Wimbo umeshatoka na unapigwa kila sehemu hakuna tamko la kukataza wimbo leo unamvua mtu cheo kisa wimbo WFK

Hili Taifa sijui lina watu wa aina gani.
 
Sio kwenye sherehe tu. Sie tuliosoma boarding tulikuwa na muziki na wanaalikwa boys kutoka shule mbalimbali tunacheza pamoja na kufurahi. Miziki ya kila aina ilikuwa inapigwa.
Hawa viongozi si juzi tu walimualika huyu Zuchu na alikuwa anaimba nyimbo hizo hizo uliwemo na huo.

Kwahiyo wao Viongozi,Zuchu kuwaimbia mubashara huu wimbo ni sawa,
Ila watoto kucheza na walimu si sawa?

Kama ni kuwajibika basi waanze kwanza kujiwajibisha.
Kama wanawaondoa walimu vyeo kwa hili tukio,basi na wao wajiondoe..

Ziara za Maadhimisho ya nishati hayana uhusiano wowote na Mambo ya Zuchu kuimba sukari Honey,,
Kama tu ilivyo kwa hao walimu.
 
Kwa Umri huo Hakuna sense hiyo

Tumesoma shule hizo hizo na tumeimba nyimbo hizohizo

Ni mawazo ngono yetu watu wazima ndiyo yanangonolize watoto
Ehh umeimba nyimbo hizo hizo au sio.
 
Sijaona kosa hapo kabisa, kuna muda wa kuburudika kidogo jamani, shule siyo vita, na hao ni watoto so hamna mawazo yoyote mabaya.
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
Safi kabisa. Nchi imepoteza mwelekeo watoto wanafundishwa nyimbo za kijinga kabisa badala ya kufundishwa elimu.
 
Kwani umefungiwa na basata hadi watoto wazuiwe kuserebuka? watoe sababu nyingine tu.
 
Wakirudi mtaani wanaimba na kina Babu sea kabis
Ss hk ndio wanakutan na maadil
 
Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
Dkt. Gwajima D
Hivi kweli huwa mnashindwa kulogic mambo madogo kama haya!😀😀 kosa la walimu lipo wapi? Au mlishaona walimu ni sehemu ya kupandia madaraja. Kila maamuzi ya mwanasiasa yapitie kwao

Hiyo nyimbo kuna mtoto nchi hii haijui?
Basata walikuwa wapi kama kunauvunjifu wa maadili kwenye huo wimbo?
Mnaelewa maana ya burudani? Mnataka wapige nyimbo za aina gani kwenye shughuri za sherehe?
Kuna maadili gani yamevunjwa hapo kwenye clip?

Viongozi Ifikie hatua mpime kabla ya kutoa maamuzi! Vile nyinyi mnavyopenda vyeo basi kila mtu anapenda. Walimu hao wasiondolewe kwenye nyazifa zao. Hawana kosa.
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
Na Viongozi na mawaziri wote waliokuwepo wakati Zuchu anatumbuiza waachie ngazi.
 
Vitu hivi
 
Mkenda kama wewe unawaza ngono si wote wanawaza kama wewe.

Jaribu kuangalia hiyo video katika mtazamo wa burudani.

Na kama kweli unajali sana maadili basi tumbuaneni mawaziri wote mliomualika juzi kati Zuchu akawa anaimba nyimbo hizo hizo tena live huku mkiacha meno yote nje kwa tabasamu.
 
Mkenda kama wewe unawaza ngono si wote wanawaza kama wewe?

Jaribu kuangalia hiyo video katika mtazamo wa burudani.

Na kama kweli unajali sana maadili basi tumbuaneni mawaziri wote mliomualika juzi kati Zuchu akawa anaimba nyimbo hizo hizo tena live huku mkiacha meno yote nje kwa tabasamu.
Nyani haoni kundule, mkuu wangu
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Aisee nilidhani unatania kumbe kweli bhana, tena mwanzoni tu mwa video.. nchi ngumu sana hii..
 
Hawa viongozi Wapuuzi wakubwa tena inaniuma sana nikiskia watoto wadogo wanatafuta hani wao huku mtaani ndio kimenuka achana na shule.Wanazuia sahiz wakati basata wali preview wimbo?Basata walipitishaje huu wimbo
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Aisee mbona hatari sana, ndio maana niliacha kusikiliza bongofleva[emoji57]
 
Mimi kama mwalimu mzoefu nachelea kusema kuwa waziri kakurupuka,shuleni sio mahali pa kujifunza ya darasani tu,kuna extra curriculum ambayo inajumlisha mambo hayo,huo wimbo wa kawaida sana,wasitake kutufanya walimu tuishi kama panya mashinoni

Kama wazirianaona hii comment imemkela na mimi anifukuze kazi,niko shule ya msingi mpigamiti wilaya ya liwale
[emoji23][emoji23][emoji23] weee
 
Back
Top Bottom