Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Halafu tunashangaa kwann siku hizi umalaya, mimba za utotoni, kuingiliwa kinyume na maumbile, ubakaji, utomvu wa nidhamu, kukosa adabu, kushuka kwa uwezo wa kufaulu na takataka zingine kushamiri katika jamii chanzo ni nini.

Sasa hawa watoto wameshika haya mashahiri ya hizi nyimbo mwanzo mwisho na wanaimba bila kukosea ila ukimuuliza mbili mara saba anababaika, watoto wanajazwa vichwa na akili haya mambo ya uchafu wa ulimwengu na walimu ambao ndio walezi na walinzi wa watoto wetu ndio wamegeuka kuwa wahamasishaji.

Kuna nyimbo nyingi sana za kusikiliza na kuwaimbisha watoto ila sio hizi za Wasafi nyimbo zilizojawa na kila aina ya mapepo ya uchafu wa kingono.

Inasikitisha sana.
 
Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.
Kosa ni aliyecheza au aliyeruhusu muziki usio na maadili upigwe public, kama music hauna maadili mbona aliyeimba hajatiwa nguvuni kwamba anapolute jamii?

Hivi wale wabunge waliocheza wimbo wa nyegezi walipokuwa Rwanda mbona hawakuchukuliwa hatua? Kwenye mabasi karibu yote kunapigwa nyimbo za nusu uchi mbele za watoto mbona mamlajpka ziko kimya
 
Uamuzi waliochukua sio suruhisho. Suruhu kubwa ni kufungia na kuzuia nyimbo hizo kuimbwa maana hazina maadili kabisaaaaaaaa! Mamlaka zinazohusika yaani BASATA walione hili na kuchukua hatua Kwa nyimbo ambazo hazina maadili. Msanii wakiume anavaa kanga Moja na kupanda jukwaani manaake Nini? Na wengine wengi kabisa
 
Hongera sana mh Waziri tusiruhusu watoto wetu wakachezeshwa Huo upupu wa Zuchu Bora ingepigwa reggae wimbo mmoja wa Bob Marley au Lucky Dude.
Unamsema zuchu Maudhui yake wakati anayoyaimba ndio unayoyafanya.. unafiki mkubwa
 
Kazi kwelikweli, badala waufungie wimbo, wanawavua walimu wakuu madaraka
 
View attachment 2801642

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.
Unajua wanasiasa ni wapumbavu sana!

Sasa kumbe wanajua kabisa kuna nyimbo zisizokuwa na maadili sasa kwanini wasizifungie kabla hazijavuja mitaani ili kuondoa hizi sintofahamu?hovyo kabisa.
 
Mimi kama mwalimu mzoefu nachelea kusema kuwa waziri kakurupuka,shuleni sio mahali pa kujifunza ya darasani tu,kuna extra curriculum ambayo inajumlisha mambo hayo,huo wimbo wa kawaida sana,wasitake kutufanya walimu tuishi kama panya mashinoni


Kama wazirianaona hii comment imemkela na mimi anifukuze kazi,niko shule ya msingi mpigamiti wilaya ya liwale
Na huko Mpigamiti.
.mna Honey honey ....😁
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni...
Mmmh hapo napingana nae profesa ametumia hisia kuliko akili. Watoto kucheza nyimbo za zuchu sio kosa ,,kisa ni misingi na mazingira yetu yakibongo mara ngapi kampeni za CCM nyiimbo za zuchu zinapigwa.
 
Back
Top Bottom