Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Ni rahisi sana kumlaumu mwingine kabla ya kuangalia namna gani kunaweza fanyika marekebisho. Na kabla ya kutoa hukumu, onyo linatakiwa kutangulia.

Na hawa jee..!!!?

Wazazi wao wavuliwe cheo cha kuwa wazazi?
Maharusi wawajibishwe?
MC avuliwe u MC
DJ apokonywe u DJ...?
Au dada wa kazi arudishwe kwao...!!!???
 
Yuko sahihi
Hatuwezi Lea wakimbia shule
Kina dayamond
Hatulei kizazi Cha wahuni
Wakimbia shule👌hapana
Mkamate Sana elimu usimwache aende zake,🙏🙏🙏
 
Ni rahisi sana kumlaumu mwingine kabla ya kuangalia namna gani kunaweza fanyika marekebisho. Na kabla ya kutoa hukumu, onyo linatakiwa kutangulia.

View attachment 2801690

Na hawa jee..!!!?

Wazazi wao wavuliwe cheo cha kuwa wazazi?
Maharusi wawajibishwe?
MC avuliwe u MC
DJ apokonywe u DJ...?
Au dada wa kazi arudishwe kwao...!!!???
MC alijiongeza akanza kuwaimbia shele yetu nzuri sana imepambwa maua...
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.

Ila asilimia 99 ya hao watoto hapo inaonesha hajawahi kuiona video ya huo wimbo vile unachezwa.
Maana watoto ninwazuri sana kwenye kunakili jambo. Ungeshaona wanainama na kupeleka viuno mbele.

Ila wote wanarukaruka na kusukumana tuu kama ule wimbo wa maua mazuri yapendeza, ukiyatizamaaa.......

Natumai walimu watarudishiwa nyadhifa zao. Walau wapewe onyo kwanza au karipio.
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
Hizi shule si zipo chini ya Tamisemi
 
MC alijiongeza akanza kuwaimbia shele yetu nzuri sana imepambwa maua...

Alishaona video ita trend na inaweza ikamfanya akakosa ugali siku zijazo.

Akarekebisha fastaa, maana wazazi na wenye sherehe ndo watakuwa walipanga watoto waingie ukumbini na huo wimbo. Ila sasa watoro wenyewe....

Zuchu anasubiri....🙄
 
na hii kuwaweka watoto kwenye sherehe sijui za harusi au kitugani zilizo jaa watumia vileo naona haiko sawa kabisa

mtoto kasikia habari ya shule kajaza mashavu kabisa
 
Yuko sahihi
Hatuwezi Lea wakimbia shule
Kina dayamond
Hatulei kizazi Cha wahuni
Wakimbia shule[emoji108]hapana
Mkamate Sana elimu usimwache aende zake,[emoji120][emoji120][emoji120]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila walimu hawana kosa jamani.
 
Back
Top Bottom