Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Kuna jambo najiuliza lakini majibu sipati. Hivi BASATA wapo kwa ajili tu ya kufungia baadhi ya nyimbo au wana wasanii wao ambao hata wakiimba nyimbo za kipumbavu hawafungiwi au wanafungia nyimbo kwa kusikiliza maelekezo kutoka juu? Mimi naona BASATA ni kama genge la wahuni na wachumiatumbo ambao hawana msaada wowote katika kusimamia sanaa bali wapo pale kwa ajili ya kufurahisha watu fulani. Maoni yangu yanaungwa mkono na serikali ambayo imewashusha vyeo walimu baada ya kuwaruhusu wanafunzi kucheza wimbo huu hapa chini ambao hauna maadili.

View attachment 2801790
Serikali imewashusha vyeo walimu hao wawili na kuwapa karipio kali baada ya kuruhusu wahuni kutoka mtaani kuja kuwachezesha wanafunzi wimbo wa kihuni. Msikilize hapa Prof Adolph Mkenda akiwashusha vyeo walimu waliohusika na uhuni huu:

View attachment 2801794
SINTOFAHAMU
Ikiwa wimbo huu hauna maadili kwanini BASATA hawajaufungia? Je, hawaoni kuwa wameshindwa kazi waondoke ofisini? Je, katika hili sakata ni nani aliyekengeuka?

1. ni serikali ambayo imewafuta vyeo walimu kwa kuchezesha wanafunzi wimbo ambao haujafungiwa na BASATA?;
2. ni BASATA walioshindwa kung'amua maudhui ya kihuni yaliyomo kwenye wimbo husika na kuufungia?; au
3. ni walimu waliochezesha wanafunzi wimbo ambao haujafungiwa na BASATA?

Kwa ujumla, kuna tatizo mahali, sio bure. Nchi hii ina mambo ya ovyo sana.
Uonevu tu, mbona vitoto vinarukaruka tu,wala havijui nini wamaimba [emoji24][emoji24][emoji1787][emoji1787]
 
Tunadhibit
Mwanangu juzi ananiimbia hizo nyimbo,nikamwuliza umesikia wapi?manake nyumbani hazipigwi na Kuna channel tumeblock,akanambia anatupigiaga dreva tukienda shule[emoji1787]nikamwambia lol nitaongea na mwalimu,akanambia , hapana usimtaje[emoji1787][emoji23]akamwonea huruma kibarua chake mzee yule
Nikamwambia,ok usiwe unazisikiliza si nzuri,akajibu sawa mama,tukamaliza[emoji120]
Mihemuko tu, Nchi ya kichawa chawa tu[emoji24]nyimbo yenyewe imekaa kitoto toto [emoji1787]
IMG_20231102_042000.jpg
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Wanatafuta kutirendiiiiiii huku wasijue kuna watoto. Hichi kizazi cha Zuchu kuna kazi ya ziada.
 
Mimi kama mwalimu mzoefu nachelea kusema kuwa waziri kakurupuka,shuleni sio mahali pa kujifunza ya darasani tu,kuna extra curriculum ambayo inajumlisha mambo hayo,huo wimbo wa kawaida sana,wasitake kutufanya walimu tuishi kama panya mashinoni

Kama wazirianaona hii comment imemkela na mimi anifukuze kazi,niko shule ya msingi mpigamiti wilaya ya liwale
Mpigamiti hauko pekeyako au afukuze wote?
 
Halafu kwenye kampeni za CCM ni nyimbo hizo hizo zitatumika kukusanya watu, yaani vitu vingine vinachekesha kweli walimu wanateseka sana nchi hii mara wachapwe, wakimbizwe kama watoto, wafanywe masanamu km hivi nao wameinama tu kama makondoo
 
Back
Top Bottom