Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

na hii kuwaweka watoto kwenye sherehe sijui za harusi au kitugani zilizo jaa watumia vileo naona haiko sawa kabisa

mtoto kasikia habari ya shule kajaza mashavu kabisa
Na hapo utakuta wameweka kwenye kadi ya mualiko watoto hawaruhusiwi, watoto waishie kanisani.

Haswa huyo mtoto aliyenyoa, anaonekana ndo mastamaindi, huyu mwingine yuko twisheni....

Hatari kabisa, malezi ni kazi.
 
Huko mtaan je?
Tunadhibit
Mwanangu juzi ananiimbia hizo nyimbo,nikamwuliza umesikia wapi?manake nyumbani hazipigwi na Kuna channel tumeblock,akanambia anatupigiaga dreva tukienda shule🤣nikamwambia lol nitaongea na mwalimu,akanambia , hapana usimtaje🤣😂akamwonea huruma kibarua chake mzee yule
Nikamwambia,ok usiwe unazisikiliza si nzuri,akajibu sawa mama,tukamaliza🙏
 
kuvuliwa wadhifa wa ukuu wa shule kwa wahusika ni umasikini wa kufikiri.!!

shida ya iyo video iko wapi?

wanafunzi kucheza wimbo wa honey? kama wimbo unakiuka maadili mbona BASATA hawajaufungia?

ni sawa na hawa watu wa usafi wanaokusanya vifungashio vya plastiki kwa wafanyabiashara kisa haviruhusiwi badala ya kudhibiti uzalishaji wa ivo vifungashio, uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

mbona kangi lugola alikata mauno hadharani na hakuchukuliwa hatua yoyote au yale ndo maadili?

shida ya hii nchi inaendeshwa kwa mihemko.!!!.
 
Unajua wanasiasa ni wapumbavu sana!

Sasa kumbe wanajua kabisa kuna nyimbo zisizokuwa na maadili sasa kwanini wazifungie kabla hazijavuja mitaani ili kuondoa hizi sintofahamu?hovyo kabisa.
Upuuzi na matumizi mabaya ya madaraka huo wimbo ni moja kati ya nyimbo zinazopendwa sana na watoto hata ukiwademote walimu wakuu unafikiria kutakua na mantiki yoyote kwa watoto?
 
Kuna jambo najiuliza lakini majibu sipati. Hivi BASATA wapo kwa ajili tu ya kufungia baadhi ya nyimbo au wana wasanii wao ambao hata wakiimba nyimbo za kipumbavu hawafungiwi au wanafungia nyimbo kwa kusikiliza maelekezo kutoka juu? Mimi naona BASATA ni kama genge la wahuni na wachumiatumbo ambao hawana msaada wowote katika kusimamia sanaa bali wapo pale kwa ajili ya kufurahisha watu fulani. Maoni yangu yanaungwa mkono na serikali ambayo imewashusha vyeo walimu baada ya kuwaruhusu wanafunzi kucheza wimbo huu hapa chini ambao hauna maadili.


Serikali imewashusha vyeo walimu hao wawili na kuwapa karipio kali baada ya kuruhusu wahuni kutoka mtaani kuja kuwachezesha wanafunzi wimbo wa kihuni. Msikilize hapa Prof Adolph Mkenda akiwashusha vyeo walimu waliohusika na uhuni huu:


SINTOFAHAMU
Ikiwa wimbo huu hauna maadili kwanini BASATA hawajaufungia? Je, hawaoni kuwa wameshindwa kazi waondoke ofisini? Je, katika hili sakata ni nani aliyekengeuka?

1. ni serikali ambayo imewafuta vyeo walimu kwa kuchezesha wanafunzi wimbo ambao haujafungiwa na BASATA?;
2. ni BASATA walioshindwa kung'amua maudhui ya kihuni yaliyomo kwenye wimbo husika na kuufungia?; au
3. ni walimu waliochezesha wanafunzi wimbo ambao haujafungiwa na BASATA?

Kwa ujumla, kuna tatizo mahali, sio bure. Nchi hii ina mambo ya ovyo sana.
 
Wimbo upite BASATA

Kwamba maudhui yake yanafaa alaf mkuu wa shule/mwl.mkuu apokee wageni (wafadhili) aanze kukagua kama wana wimbo wa Zuchu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1430]
Alaf mawaziri wapo serious wanatoa matamko[emoji1787][emoji1787][emoji1430]

Haki nchi hii kuna uhaba wa viongozi basi tu siwezi kuandamana[emoji1241]
 
me naona bado wanaendelea kung'amua maudhui katika hii nyimbo.hiyo ndo tafsri rahisi
 
Dah yani nyimbo wanafunzi wanaiimba wenyewe kwa furaha imekuwa tatizo tena kwa walimu wakuu?

Af wanafunzi wote wanaiimba it means wanaijua na sidhani kama shule ndiyo inawafundisha wanafunzi nyimbo hizi.

Angalieni ufaulu wa wanafunzi kabla ya kuwahukumu walimu wakuu kwa namna hii.
 
Back
Top Bottom