Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Sijui labda macho yashakuwa ya uzee tena.... lakini sijaona kosa hapo la kufikia wakuu wa shule kuvuliwa vyeo tena ikiwa mari kutoka kwa waziri 🙁
Tena walimu wenyewe wanacheza kawaida tu

Hata watoto wanaonyesha kufurahia

Itakuwa mkenda mawazo yake machafu anadhani kila mtu anayo.
 

Na kwanini upeleke watu kwenye tafsiri?. Kwani huwezi kuimba vitu vya kueleweka?
 

Viongozi wanazingua.
 
Kizazi Cha Sasa ni Cha nyoka. Waziri angeacha watu wajifanyie wanavyo taka. Maana Kuna kipindi BASATA walikuwa walifungia nyimbo watu wanawaijia juu. Pia sio kwa ubaya, kwanini wasanii watu wanapenda kuimba matusi na mambo ya chumbani?. Mbona akina Prof J, Mr Two, Wagosi wa kaya waliwika Sana bila kuimba matusi. Leo nyimbo zote zinafanana na hakuna ubunifu.
 
Sijui ni mazingira ya eneo husika au laah! Binafsi huwa sipendi na huwa sifuatilii nyimbo za bongo fleva kwa sasa mimi ni mpenzi wa bongo fleva mongwe na zilipendwa za akina TX Moshi. Ila kwa kuwa dunia imebadilika muziki kwa sasa ni biashara na kuna mpango wa kuanzisha masomo ya amali mashuleni ambayo pia yatachukua na huo muziki, sijajua huo muziki utakao takiwa kufundishwa utazingitia soko la sasa la dunia au laah!
 
Atiiii... WTF
 
Naunga mkono waziri, kama ingekuwa ni shule yangu binafsi hao walimu nafukuza kazi. Lazima utofautishe nyimbo za shuleni zenye maadili na zile za kihuni
 
Mh waziri yupo sahihi , mtoto ukimpasua ubongo na Akili ni gharama kubwa kumrejesha katika reli .

Natamani Wcb wajitafakari Sana pia wazazi na walimu ipo sababu ya kuacha ubinafsi na kuwa na utu , UPENDO na moyo wa Huruma kuhusu hiki kizazi ili kisipotee mazima.

Nipo temeke niseme watoto wanapotea kwa kasi kubwa Sana .😒🤢
 
Badala ya kufungui miziki ya hovyo unawvua nyadhifa walimu
 
Kosa la Walimu lipo wapi?

Nimesikiliza, watoto wanajua kila neno na mistari ya wimbo tena kwa kufuata midundo.
Wanaimba kwa pamoja bila kukosea, na wanacheza kwa mirindimo sawia

Watoto walijua huu wimbo kutoka majumbani kwao. Hao wazazi wanaolalamika walikuwa wapi?

Kilichotokea hakina uhusiano na Walimu, kinatuonyesha ubovu wa malezi majumbani kwetu! tuanzie huko

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Hizo hazina shida,kuimba matatizo ya jamii ndiyo mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…