LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Huo wimbo unapendwa sana kuimbwa na watoto hata wale wachanga ambao hata shule ya awali hawaanza. Kama mnaona huo wimbo hauna maadili upigeni ban. Kuna kigogo mmoja mtu mzito wa hadhi ya juu alikwenda uganda kikazi. Katika mambo ya kuburudisha wageni ukawekwa wimbo uliopigwa marufuku nchini na yeye akaserebuka kisawasawa kana kwamba hajui huo wimbo kuwa ulifungiwa. Ni ule wimbo wenye neno la stendi kuu ya mabasi ya mikoani Mwanza ila sio Buzuruga. Mind kwamba wimbo huo wa honey ni wa mburudishaji wa chama chao katika matukio yao hasa kampeni zao. Ina maana siku kampeni zikianza muimbaji huyo hataimba wimbo huo pendwa na wenye hamasa kubwa kuvutia wananchi kwenye kampeni zao?