Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Tunajadili mikojo wakati tukisubiri treni za umeme.
 
kwema Wakuu!

Tuachane na mambo ya Ukraine na Urusi.
Leo sitaki kupotezea muda watu.

Moja ya mambo yaliyonishangaza tangu nilipotoka nyumbani miaka 10 iliyopita ni kuona wakazi wengi kuwa na tabia ya kukojolea kwenye makopo au ndoo nyakati za usiku.

Hivi inakuwaje mtu alale na Mikojo wakati haumwi?
Ni uvivu wa kutoka nje usiku au ni Woga?

Kinachoshangaza zaidi ni kuona tabia hii ipo mpaka Kwa wanaume. Hivi mwanaume mzima unakojolea kwenye kopo au ndoo kweli badala ya kutoka nje na kujisaidia chooni.

Unakuta mtu kaoa kabisa alafu yeye na Mke wake wanakojolea kwenye ndoo au kopo. Kwa kweli hili sio uungwana Kabisa.

Halafu ndoo hiyo hiyo ati mtu anaogea au kufulia😀😀 hii kuna uchafu zaidi ya huu? Ukimuuliza atakwambia ati ndoo ameiosha, upuuzi mtupu.

Uchunguzi huu unawahusu zaidi Wale wenye nyumba za kupanga ambazo sio Self-container, isipokuwa Choo kipo Kwa nje kimejitenga.

Pia baadhi ya wenye nyumba ambao vyoo vyao vipo Kwa nje.

Ushauri wangu, unapoenda ugenini kusalimia uwe Makini sana, unaweza ukadhani unaoga kumbe unajipaka mikojo ya watu japokuwa watakuambia wanaisafisha hiyo ndoo.

Mikojo na mavi no uchafu, ni najisi, watu lazima muwe wasafi bhana sio muwe Kama majini.

Wito: wenye tabia hii nawasihi mubadilike, acheni kukojolea kwenye makopo au ndoo, alafu ndoo hizohizo mnaogea na kufulia nguo. Huo ni UCHAFU.

Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Buza, Dar es salaam
Kama kweli unajuwa hali ya vyoo vya nyumba za kupanga usingeuliza hili. Kuna vyoo vingine ni vibovu, vichafu, vinatoka funza, wengine hushusha zigo juu, na zaidi yote havina usalama.

Unaweza kutumbukia chooni kirahisi. Sasa ukitumbukia usiku nani atakuokoa?

Wengi wanatmia makopo/ndoo kwa kulinda usalama na afya zao.
 
Sasa ndo nimepata majibu kwenye hii mada...zamani Kuna mahali nilikua naishi ,nilikua nasikia kila ikifika saa sita au Saba usiku lazima nisikie kelele za michirizi ya kitu Kama maji hivi yakimiminika kwenye ndoo au beseni Tena kwa Kasi Sana hapo chumba Cha jirani,kila siku najiuliza hiyo michirizi ya maji kila siku ninayoisikia chumba Cha jirani (mwanamke)ni vitu gani haswa...nimepata jibu Sasa,lakini choo kilikua kipo ndani ya fensi kabisa siyo nje...
Sasa mfano mmejipigia bia za kutosha,au mmekunywa maji mengi wakati wa dinner,choo kipo nje huko mbali...

Kuna wengine ndoo ya lita kumi inajaza mkojo robo tatu ya ndoo.

Ukisema uende chooni hutalala aisee usiku mzima utafanya kazi ya kenda rudi.

Ukiwa ndoo lako unashuka kwa bed unaachia mzigo unalala.

Asubuhi ya mapemaaaa unawahi kabla watu hawajaamka unaenda kumwaga.

Sasa ole wako ujisahau upige teke bahati mbaya kojo limwagikie ndani ya nyumba..
[emoji28][emoji28]
 
Na kwanini uamke usiku kukojoa katika hali ya kawaida ukitoa watoto, wajawazito na wale wenye tezi dume au kisukari, wagonjwa wa Pressure wanaotumia diuretics, au waliokunywa pombe, binadamu wa kawaida akisha kojoa kabla ya kulala huwa ana uwezo wa kulala mpaka kunakucha bila kuhitaji kukojoa! Km wewe unalala kuanzia saa 4 usiku unaweza kuhimili mkojo mpk kufikia saa 12 Asubuhi.
Kama umekunywa maji mengi...utaamka tu ukojoe
 
Kama kweli unajuwa hali ya vyoo vya nyumba za kupanga usingeuliza hili. Kuna vyoo vingine ni vibovu, vichafu, vinatoka funza, wengine hushusha zigo juu, na zaidi yote havina usalama. Unaweza kutumbukia chooni kirahisi. Sasa ukitumbukia usiku nani atakuokoa? Wengi wanatmia makopo/ndoo kwa kulinda usalama na afya zao.


Ikiwa ni hivi, nini kinawashinda wasiboreshe vyoo na kuviweka katika Hali ya Usafi?
 
Sasa mfano mmejipigia bia za kutosha,au mmekunywa maji mengi wakati wa dinner,choo kipo nje huko mbali...
Kuna wengine ndoo ya lita kumi inajaza mkojo robo tatu ya ndoo.
Ukisema uende chooni hutalala aisee usiku mzima utafanya kazi ya kenda rudi.
Ukiwa ndoo lako unashuka kwa bed unaachia mzigo unalala.
Asubuhi ya mapemaaaa unawahi kabla watu hawajaamka unaenda kumwaga.

Sasa ole wako ujisahau upige teke bahati mbaya kojo limwagikie ndani ya nyumba..
[emoji28][emoji28]
Mnaishi maisha ya kimasikini sana lakini mtu akikuta uko sehemu umekaa umechongoa mdomo kuwasema watu utafikili umejitosheleza kwa kila kitu.....
 
Back
Top Bottom