Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
- Thread starter
-
- #101
I naelekea unapenda sana porojo,lete hoja tujadili na sio bla blah blahWatu pekee wanaoweza kufanunua uwepo wa Mungu bila jazba ni Wakristo hutumia Pschology & Theology pana kukuelewesha hadi ukaingia kwenye mfumo kumuamini Mungu wao Yahweh.. vinginevyo kutana na wale kutoka Tandale kwa Tumbo waumini wa Masjid Khomenei, ukibishia kuhusu mungu wao aitwae Allah uwe na mbio kama Ussain Bolt vinginevyo watakumwaga utumbo na kukutenganisha viungo wapate thawabu kwa mungu wao Allah
Madhara ya kutokujibu kwa mda mrefu unaona uvivu wa kurudi nyuma bwashee 😁Bwashee ebu nyosha maelezo,hoja yako iko wapi hapa?
Hili si jambo geni kulisikia kutoka kwenu,mara nyingi mnasema inakuwaje Mungu muweza wa yote,mwenye upendo aruhusu vita au mauaji na mambo kama hayoUkishakuwa na mjadala kujadili uwepo wa Mungu tu, hususan Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote, mjadala huo tu nao ni ushahidi kuwa Mungu huyo hayupo.
Kwa sababu, kwa sifa zake hizo, Mungu huyo angekuwapo, angejulikana na viumbe wote, popote, muda wowote, bila utata, kwa namna ambayo haihitaji mjadala na mjadala hauwezekani.
Hivyo, mjadala huo, kwenye ulimwengu ambao Mungu yupo, usingewezekana kuwepo.
Hili ni jambo rahisi tu kuelewa.
Lakini unaweza usielewe.
Na usipoelewa pia ni ushahidi kuwa huyo Mungu hayupo.
Kwa sababu huyo Mungu, kama yupo, atakuwa si mkatili hivyo akunyime uelewa ndogo tu huu.
Potezea isiwe tabuMadhara ya kutokujibu kwa mda mrefu unaona uvivu wa kurudi nyuma bwashee 😁
Kama binadamu walitokea tu kama unavyosema from nowhere kwanini hawakuendelea kutokea kwa stahili hiyo mpaka leo, kipi kilifanya tuzaliane?Hakuna binadamu wa mwanzo.
Kama kungekuwa na binadamu mmoja tu wa mwanzo kwa binadamu wote ulimwenguni, basi kusingekuwa na utofauti wa rangi na vinasaba kwa binadamu.
Binadamu wote tungefanana kwa rangi na vinasaba, kwa sababu tumetokana na Binadamu mmoja tu.
Lakini sivyo, binadamu tunafoutiana rangi na vinasaba.
Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, wajapani, wafilipino, wakorea, wahindi weusi, wahindi weupe, waarabu n.k
Sasa kwa huu, utofauti wa rangi na vinasaba HAIWEZEKANI binadamu wote tuwe tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo.
Kama binadamu wote, tungekuwa tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo, tungefanana kwenye kila kitu.
Karibu utuelimishe ndugu yetuMleta hoja na wajibu hoja nadhani wote kuna haja kwenda kusaka references kwanza maana naona nyote humu it's pointless,,,, natamani kuwajibu lakini ngoja niwaandalie uzi wenye kila utamu
NakaribiaKaribu utuelimishe ndugu yetu
Duh unaamini imani yako ya Mungu ni sahihi Kuliko ya wengine ?Huwa nikimsikia mtu tu anasema au anaamini kuna miungu wengi ambao wamefanya mambo mbali mbali huwa moja kwa moja inaonyesha hamjui Mungu
umewahi kubahatika kusoma vitabu vya Dini zingine ambazo sio IBrahimic religion?Kama binadamu walitokea tu kama unavyosema from nowhere kwanini hawakuendelea kutokea kwa stahili hiyo mpaka leo, kipi kilifanya tuzaliane?
Sijawahi kusoma,nitafurahi kama utaweka mchango wako hapa tujifunze,lengo ni kufahamishana na kuelimishanaumewahi kubahatika kusoma vitabu vya Dini zingine ambazo sio IBrahimic religion?
umewahi kusoma BUdha au shinto?
au Summerian?
je unajua kuwa Uhindu ni dini ya zamani sana kuliko dini yoyote ya Ibrahimic religion?
Ni kwamba its Coincidental tumezaliwa kwenye dini au madhebu tuliyopo sio by choice ni only by chance iliyotuchagua kuwa huko pemgine leo hii ungezaliwa china ungekuwa tayri kufa kutetea shinto na kuona ibrahimic religion ni uongo au kutetea Budha and etc..Sijawahi kusoma,nitafurahi kama utaweka mchango wako hapa tujifunze,lengo ni kufahamishana na kuelimishana
Binadamu hawatokei, Binadamu wanazaliwa.Kama binadamu walitokea tu kama unavyosema from nowhere
Kujamiiana(sex) ndio kunafanya tuzaliane.kwanini hawakuendelea kutokea kwa stahili hiyo mpaka leo, kipi kilifanya tuzaliane?
Mbona kama unaleta janja janja,ok tufanye kwamba hujasema binadamu wanatokea, kuzaliana kulikuja baadae baada ya kuwepo asili ya mwanadamu na ndio wakaanza kuzalianaBinadamu hawatokei, Binadamu wanazaliwa.
Hakuna sehemu nilikwambia Binadamu wanatokea.
Binadamu wanazaliwa kwa kuzaliana wao kwa wao.
Kujamiiana(sex) ndio kunafanya tuzaliane.
Hata wewe ulizaliwa kwa sababu Baba na Mama yako wali sex.
Kwa nini unafikiri kuzaliana kulikuja?Mbona kama unaleta janja janja,ok tufanye kwamba hujasema binadamu wanatokea, kuzaliana kulikuja baadae baada ya kuwepo asili ya mwanadamu na ndio wakaanza kuzaliana
Asili ya Binadamu ni binadamu mwenyewe.Hoja hapa je huyo binadamu wa kwanza asili yake ni nini?
Kwanza nakubaliana na maelezo yako kwamba ni kweli kabisa wengi wetu tumejikuta kwenye imani hizi kutokana na kujikuta humo kwa mpango ambao tumeukuta,ni wachache sana ndio wamebadilika baada ya kusoma na kuchambua na kuridhishwa na hoja na taarifa za dini hizoNi kwamba its Coincidental tumezaliwa kwenye dini au madhebu tuliyopo sio by choice ni only by chance iliyotuchagua kuwa huko pemgine leo hii ungezaliwa china ungekuwa tayri kufa kutetea shinto na kuona ibrahimic religion ni uongo au kutetea Budha and etc..
lengo langu ni nini na kwanini nasema hivyo..
umezungumzia story ya uumbaji lakini hujafanya research kugundua kuwa story ya uumbaji uliyonayo ambayo unaiamini inafnaya kazi only in ibrahimic religions ila ukiama dini tu wana hadithi zao za uumbaji na hawana kiumbe anaitwa Adam wala hawa na wamekuwa wakiamini hivyo kwa miaka zaidi ya 3000 kabla ya kuzaliwa kristo na kabla ya dini ya kiyahud..
sijaiweka coincidental bahati mbaya just imagine ertugrul ungezaliwa roma italy au ungezaliwa vatican leo hii ungekuwa unaupinga uislam na hivyo hivyo kama ungezaliwa Kwa wayahudi ungekuwa unaupinga uislam na ukristo kwa nguvu zako zote..
sasa Hiyo tafsiri ya UUngu au Mungu bado imetofautiana kwenye kla dini kuna wengine wana Mungu mmoja kuna wngine wana mungu watatu na kuna wengine wanakataa mungu huyu sio wao etc..
so dhana ya Mungu its school of thought + coincidental na ni very contradictory facts na according to arristaote law of contradiction iliyopo kwenye kitabu chake cha metaphysics...Ina cancel tukio zima la uwepo mpaka tuchunguze vizuri....
so Tuanze mada mimi na wewe kama hutojali ertugrul unaweza kuthibitisha uwepo??
dizani ya kujibu hoja na kuchangia tutajifunza mengi
Kwa nini unafikiri kuzaliana kulikuja?
Kwa nini hufikirii kuzaliana kumekuwepo milele?
Je ni lazima kwamba kuzaliana kuwe kulikuja?
Je kuzaliana hakuwezi kuwepo bila kuja?
Asili ya Binadamu ni binadamu mwenyewe.
Binadamu wanazaliana wenyewe kwa wenyewe na ndio asili ilivyo.
Unataka asili gani nyingine?
Nilishakwambia hakuna binadamu wa kwanza duniani kwa binadamu wote.
Na hili linathibitika kwa kuwepo binadamu tunao tofautiana rangi na vinasaba.
Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea, wahindi weusi na weupe n.j
Sasa kwa huu utofauti, Haiwezekani binadamu wote tuwe tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo.
Kama ingekuwa binadamu wote ulimwenguni tulianzia kwa binadamu mmoja tu wa mwanzo, basi tungefanana kwenye kila kitu. Rangi na vinasaba.
Ni kujidanganya kusema binadamu wamezaliana milele,lazima kuna mbegu ambayo ilikuwepo hapo awalSikupenda kabisa kugusia upande wa maandiko kwakuwa nyie hamuamini maandiko,lakini itoshe kusema kuna mambo sayansi haiwezi kuelezea,ndio maana unapata tabu kujua kwanini kuna wahindi,wazungu,waafrika au Any colorHapa dini ina majibu yake,kwamba tumeumbwa kwa mataifa ili tufahamieni tu lakini katika wote hao mbora wao ni mchamungu tuKwahiyo kwa sayansi kushindwa kuthibitisha kwanini kuna waupe weusi au brown haimaniishi kwamba asili yetu sio mojaHapa kuna hoja kuu nne zinazotumika kutetea chanzo cha Mungu:
1. Hoja ya Kosmolojia (Kalam Cosmological Argument)
Hoja hii inajikita katika kanuni ya sababu na athari. Inasema kuwa kila kitu kilichokuwa na mwanzo lazima kiwe na sababu iliyokisababisha.
Ulimwengu una mwanzo: Sayansi ya kisasa (kama nadharia ya Big Bang) na sheria za thermodynamics zinathibitisha kuwa ulimwengu haukuwepo milele; una mwanzo.
Sababu ya kwanza: Ikiwa ulimwengu una mwanzo, basi kuna kitu "nje" ya ulimwengu (nje ya muda, nafasi, na mata) kilichousababisha. "Kitu" hicho ndicho kinachoitwa Chanzo cha Kwanza au Mungu.
2. Hoja ya Ubunifu na Mpangilio (Teleological Argument)
Hoja hii inaangalia utata na uratibu uliopo ulimwenguni. Ulimwengu hauonekani kuwa wa bahati mbaya, bali unaonyesha mpangilio uliokusudiwa.
Marekebisho Maalum (Fine-Tuning): Sheria za fizikia (kama nguvu ya mvuto au kasi ya kutanuka kwa ulimwengu) zimekaa katika uwiano sahihi sana kiasi kwamba kama zingebadilika kidogo tu, uhai usingewezekana.
Mfano: Kama vile saa inavyoonyesha uwepo wa fundi saa, ulimwengu changamani unaonyesha uwepo wa Mbunifu Mkuu.
3. Hoja ya Maadili (Moral Argument)
Hoja hii inahusu uwepo wa maadili ya kweli na ya kudumu (objective moral values).
Binadamu wote wana hisia ya ndani kuhusu "zuri" na "baya" (kama vile kukubali kuwa kudhulumu wasio na hatia ni kosa).
Ikiwa hakuna Mungu au chanzo cha juu cha mamlaka, basi maadili yanakuwa ni maoni tu ya watu au matokeo ya mageuzi ya kijamii. Uwepo wa sheria za kimaadili zinazofanya kazi kote duniani unaashiria uwepo wa "Mtoa Sheria" mkuu.
4. Hoja ya Ontolojia (Ontological Argument)
Hii ni hoja ya kimantiki zaidi inayotokana na dhana ya ukamilifu.
Inasema kuwa Mungu anatafsiriwa kama "Kiumbe mkuu ambaye hakuna mwingine mkuu zaidi yake anayeweza kufikirika."
Kuwepo katika uhalisia ni "kuu" zaidi kuliko kuwepo katika fikra tu. Kwa hiyo, ikiwa tunaweza kufikiria kiumbe mkuu kuliko wote, lazima kiumbe huyo awepo katika uhalisia, vinginevyo hatakuwa "mkuu kuliko wote."
HapanaHili si jambo geni kulisikia kutoka kwenu,mara nyingi mnasema inakuwaje Mungu muweza wa yote,mwenye upendo aruhusu vita au mauaji na mambo kama hayo
Hii inaonyesha kwamba mnamuweka Mungu kwenye daraja la binadamu,kwakuwa wewe una huruma,haupendi machafuko au vita au ukatili basi nawe unamuweka Mungu kwenye viwango hivyo hivyo,hapa mnaonyesha udhaifu wenu wa utambuzi na kufikir, mna la kujifunza zaidi
Kuna kitu kimoja Theists wengi na Attheists pia wote hawakielewi, vizuri.Nani ana mwamini Mungu yupi , ni sababu moja wapo ya uwepo wa Mungu kutiliwa shaka