Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Ukweli ni kwamba chini ya CCM ufisadi haukuwahi kwisha wala kupungua, huwa unaongezeka tu ila kwa mtindo tofauti.
Kama kuna ufisadi wa kutisha uliwahi kufanyika basi kipindi cha Magufuli huenda ndio kilivunja rekodi kwa mujibu wa taarifa rasmi za serikali kupitia report ya CAG, utawala wa Magufuli ulifisadi kila kitu mpaka kura za wananchi. Huyo jamaa hakuwa na woga wala aibu wakati wa kufisadi. Yaani bunge, mahakama, vyombo vya habari na vyombo vya dola vyote viliwekwa mfukoni mwake ili kufunika ufisadi wote uliokuwa unaendelea ndani ya serikali yake.
Utawala wa sasa wa Samia Suluhu nao ni utawala wa kifisadi, tena ufisadi rasmi. Tofauti pekee ni kuwa umejaribu kwa kiwango fulani kidogo kuweka wazi taarifa za mwenendo wa ufisadi unaondelea ndani ya serikalini kitu ambacho Magufuli hakutaka na hakukipenda.
Dawa pekee ya kuua mfumo mzima wa ufisadi katika nchi yetu ni kuitoa CCM madarakani.