Ukiona mtu anashabikia sana Simba na Yanga kuwa naye makini, wengi hawana akili timamu

Ukiona mtu anashabikia sana Simba na Yanga kuwa naye makini, wengi hawana akili timamu

du! ulieanzisha uzi huu utakuwa na iQ ndogo sana ........japo bahati mbaya sina muda mzuri wa kukuelezea kwa nini nakuhisi una akili ndogo hivi pole sana!!!!
 
halafu nina wasiwasi kupitia mpira huhuu lazima kuna kitu ulitendewa kikakuharibu kisakolojia ndo maana hupendi kusikia mambo ya ushabiki
 
Hapo ni kuingilia uhuru wa watu,.....na kwa namna hyo tu ww hufai kuwa kiongoz kweny taasisi yyt maana utataka wafanyakaz wafanye jambo kwa kufuata matakwa yako...nna hofu hata familia yako imekosa furaha kutokana na mtzamo wako ulivyo
 
Kwa uchunguzi mdogo niliofanya nimegundua kuwa watu wanazi sana wa hizi timu huwa hawako timamu kichwani.

Ukiona mtu muda wote au zaidi ya asilimia 70 ya maongezi yake ni Simba na Yanga. Muda mwingi anashinda amevaa jezi ya Yanga au Simba. Mitandaoni anafuatilia sana habari za Simba na Yanga. Mara Mukoko hivi, mara Manara vile, kuwa naye makini sana. Usimuamini kwa jambo la msingi. Huwa hawana mawazo ya maana. Hawana maongezi ya maana. Na mbaya zaidi wengi huonyesha dalili ya matatizo ya akili.

Jiepushe na watu wa namna hiyo.
Cc Mightier OKW BOBAN SUNZU etc
 
Kitaalam binadamu ni lazima atakuwa kuna kitu anakipenda sana hata kufikia kuwa kero kwa baadhi ya watu wengine. Hupendi mpira sawa ila jichunguze kuna uwehu flani upo, huko kunaitwa kupenda
Pamoja na hayo, kutopenda kwangu mpira kulinifanya nijione tofauti sana hasa ukizingatia wengi wanaupenda mpira. Mbaya zaidi unakuta mechi inaendelea alafu mtu from nowhere anakuuliza ngapi ngapi?
 
Jumlisha na wale wanaopenda movie za kutafsiriwa

Hahaha! Unakuta sehemu ambayo actor anamlalamikia boss wake kutokuwa na mbinu mpya ya kuinua kampuni, utamsikia mtafsiri “ Mama mkwe mkanye mwanao nitakuja kumfumua fumua”
 
Kwa uchunguzi mdogo niliofanya nimegundua kuwa watu wanazi sana wa hizi timu huwa hawako timamu kichwani.

Ukiona mtu muda wote au zaidi ya asilimia 70 ya maongezi yake ni Simba na Yanga. Muda mwingi anashinda amevaa jezi ya Yanga au Simba. Mitandaoni anafuatilia sana habari za Simba na Yanga. Mara Mukoko hivi, mara Manara vile, kuwa naye makini sana. Usimuamini kwa jambo la msingi. Huwa hawana mawazo ya maana. Hawana maongezi ya maana. Na mbaya zaidi wengi huonyesha dalili ya matatizo ya akili.

Jiepushe na watu wa namna hiyo.
In this current life, never take everything seriously. Especially in social network life
 
Back
Top Bottom