NAWATAFUNA
JF-Expert Member
- Nov 14, 2019
- 13,284
- 24,047
Ndio hivyo wabongo tulivyo,ni hulka ambayo ipo,sio kwenye mpira tu,hata upande wa siasa.Binadamu wana mambo mengi na wanatakiwa kuwa na kiasi kwa kila jambo hasa mwanaume. Unatakiwa ukikaa na watu uweze kuwa na mazungumzo ya aina mbalimbali. Sasa wewe mtaa mzima au ofisini wanajua wewe ni mtu wa mpira, mzungumza mpira muda wote.
Wakikuona tu wanaanza kukuchonoa na habari za mpira. Na wewe unaanza kutiririka ukifikiri sifa. Kumbe wanakuona hamnazo na hawana jambo lingine la kuzungumza na wewe.
Watu wakikutana kazini asubuhi kifungua kinywa ni habari za siasa.