Wakatoliki hupenda maombi ya kujionyesha sana hasa maaskofu wao
Hivyo vifungu ukivyo nukuu ni vya agano la kale .Kuna tofauti kwenye maombi ya agano la kale ni jipya farisayo mkubwa wewe
Kanisa limeanza agano jipya .
Kwenye maombi ya agano jipya Yesu aliagiza yawe sirini sio kupiga tarumbeta mabarabarani na njia panda kuwa ooh tutakuwa na maombi ya Taifa
Huo ni ufarisayo.Mungu hasikilizi maombi ya kifarisayo kwenye agano jipya.Yakiwemo hayo ya kifarisayo ya katoliki na wapuga filimbi wa Hamelini wenzao akina Gwajima nk
Kitabu cha matendo ya mitume kipo kwenye agano katikati au?
Pentekoste β Mitume na wanafunzi wakiwa pamoja
Matendo 1:14: Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali pamoja na wanawake na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
Matendo 13:1-3: Katika kanisa la Antiokia, walipokuwa wakihudumu na kufunga, Roho Mtakatifu alisema wamtoe Barnaba na Sauli. Wote wakaomba, kufunga, na kuwawekea mikono, kisha wakawatuma.
Yesu alipokuwa anawaombea makutano hiyo ilikuwa ni sirini?
Tatizo lenu walokole ni uelewa hafifu heri wasabato mnaweza kukaa naye mkajifunza kitu na mkaelewana lakini si ninyi mnakalilishwa sana na kuamini ili hali ninyi ndo mnaenda kwenye senta na vipaza sauti mnaanza kupigia watu kelele.
Ninyi ninyi ndo mnaenda stend kuombea watu ovyo ovyo nk.
Yesu alisema utoapo sadaka hata mkono wako wa kushoto usijue kwa mujibu wa andiko hili yesu alimaanisha nini?
Mfano aliutoa yesu kwa mafarisayo ni kama leo hii uwe kwa waislamu hasa unapofika mwezi wa Ramadan.
Yaani ile funga yao hadi bidhaa zinapanda hata ukiwa na muislamu kwako familia yote itajua na hata majirani watajua kwa fln kuna muislamu na amefunga!
Hizi ni baadhi ya sifa za mafarisayo na ndio maana yesu aliwaita wanafiki.
Walikuwa wepesi kuhukumu wengine (Yohana 7:47-49).
Walikuwa wagumu kwa wengine, wakiweka mizigo ya sheria, lakini wao wenyewe hawakuyafuata kwa moyo (Mathayo 23:4).
Walizingatia sana sheria za nje, lakini wakapuuza mambo ya muhimu zaidi kama rehema, haki, na imani (Mathayo 23:23).
Walijiona wenye haki kuliko wengine (Luka 18:9-14: mfano wa Mfarisayo na mtoza ushuru).
Kwa hiyo Mafarisayo walikuwa ni watu wa dini walioonekana wacha Mungu, lakini mara nyingi walionyesha majivuno, unafiki, na kutafuta sifa, badala ya unyenyekevu na utii wa kweli kwa Mungu.
Hayo yesu aliyajua kwa sababu alikuwa Mungu alikuwa nauwezo wa kutambua kilicho ndani ya moyo wa mtu yaani nje na ndani yesu alikuwa anaona maana alikuwa na uwezo huo!
Mara kadhaa aliwaambie wasafishe vikombe kwa ndani kwanza ndipo na nje vitakuwa safi!! Maana wale watu aliwajua nje ndani.
Sasa wewe na mtoa uzi mmewatambuaje kuwa hawa madre na maaskofu ni wanafiki?
Je kama maombi yao Yana maanisha na Mungu akayajibu?
Wewe ni nani hasa hadi utambue kuwa haya maombi hayapokelewi ikiwa tu hata malaika hama Access ya kujua hilo wewe unajuaje?
Mbona Paulo aliwatanganzia waalike watu kwa ajiri ya maombi ya sabato ya pili yake?