Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Waache watu na Imani zao na ww Baki na Imani Yako,heshimu Imani za watu you are not a "god" to judge.
Acha dhihaka.
Your assertion is deeply misplaced. To expose error is not to desecrate faith, but to uphold truth. Genuine reverence for God does not consist in tolerating falsehood, but in discerning between light and darkness. Judgment belongs to God, yet Scripture enjoins His children to test every spirit, to rebuke iniquity, and to defend sound doctrine. To remain silent in the presence of deception is not humility, but complicity. Therefore, I shall not be deterred by the accusation of mockery, for it is written: 'Have no fellowship with the unfruitful works of darkness, but rather reprove them.'
 
Kuna wakati Mungu ni kiziwi. Quote yako haina uhalisia, ni mara ngapi mlisimamisha shingo wakati wa corons na kuomba? Mlijificha, Mungu gani hataki watu wajue kama unaomba kitu fulani?? Nini tofauti ya kusali na kuomba??
Soma tena Mathayo 6:6:
“Bali wewe uombapo, ingia chumbani kwako, ukishafunga mlango, mwombe Baba yako aliye sirini; naye Baba yako aonaye sirini, atakujibu"

Jifunze pia kwa Yesu. Alipotaka kuomba, alikuwa anaenda mlimani mahali pasipokuwa na watu.
Luka 5:16
“Lakini yeye alijitenga akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba.”
 
Maombi ya kujionesha ni hali ya kuomba au kufanya sala kwa kutaka watu waone, waseme na kusifia. Ni maombi ya mtu anayetafuta heshima ya kidini, sifa au umaarufu wa kijamii kwa kutumia jina la Mungu. Mtu anapotangaza mitandaoni ratiba za maombi yake na kupiga kelele “leo siku ya kwanza ya novena, sala yetu ni very powerful, leo siku ya tatu - tunaomba mfululizo, leo tunahitimisha…” huko ni kujionesha; ni kutaka watu wamwone kuwa ni mtu wa kiroho. Ni sawa kabisa na wanafiki aliowasema Yesu kuwa hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.

Yesu Kristo alisema waziwazi katika Mathayo 6:5:
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.”

Maombi ya kujionesha, yanaishia barabarani na mitandaoni tu, hayafiki mbinguni. Na mtu anayejionesha tayari amepata thawabu yake. Thawabu yake ni pongezi za watu, ‘likes’ ‘positive comments’ na kuonekana mtakatifu machoni pa wanadamu.
Punguani wahed
 
Punguani wahed
Resorting to derogatory invective rather than engaging with the substance of the argument betrays the poverty of one’s reasoning. An ad hominem barb cannot substitute for rational discourse
 
Bado hamjasema.
Tulia ndugu, Novena ni kisulisuli kitapita nanyi
Hahaa, maombi ya kulaani ndio kabisa hayasikiwi
Rum 12:14-21
"Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani."
 
Acha dharau wewe na madhehebu ya watu..unajikuta ww ndo upo sahihi kila kitu? Mbona nyie mnatupigia mikelele mitàani huko na majukwaani kwenye mikutano yenu?
 
Hahaa, maombi ya kulaani ndio kabisa hayasikiwi
Rum 12:14-21
"Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani."
Hata shetani alipomjaribu Yesu alitumia maandiko.

Rudi nyuma yangu shetani maana wewe huyawazi yaliyo ya Mungu
 
Maombi ya kujionesha ni hali ya kuomba au kufanya sala kwa kutaka watu waone, waseme na kusifia. Ni maombi ya mtu anayetafuta heshima ya kidini, sifa au umaarufu wa kijamii kwa kutumia jina la Mungu. Mtu anapotangaza mitandaoni ratiba za maombi yake na kupiga kelele “leo siku ya kwanza ya novena, sala yetu ni very powerful, leo siku ya tatu - tunaomba mfululizo, leo tunahitimisha…” huko ni kujionesha; ni kutaka watu wamwone kuwa ni mtu wa kiroho. Ni sawa kabisa na wanafiki aliowasema Yesu kuwa hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.

Yesu Kristo alisema waziwazi katika Mathayo 6:5:
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.”

Maombi ya kujionesha, yanaishia barabarani na mitandaoni tu, hayafiki mbinguni. Na mtu anayejionesha tayari amepata thawabu yake. Thawabu yake ni pongezi za watu, ‘likes’ ‘positive comments’ na kuonekana mtakatifu machoni pa wanadamu.
Mbona nyie walokole mnasali kwa kupiga makelele na pia kutumia maspika makubwa, Hayo sio maombi ya kujionyesha?
 
Uzuri wewe sio Mungu.
Na maombi yale yenu ya kilokole kupiga mikelele na kuomba kwa mic mpaka mtaa wa 10 wanawasikia kwan huko SIO KUJIONYESHA?
Kwani mimi umeona wapi nawatetea hao. Ujumbe huu unawahusu watu wote. Hata walokole kama wanaomba ili kujionyesha, maombi yao hayasikiwi. Period
 
Hujanielewa. Mada yangu inawahusu wanaoomba novena huku wakijigamba kwa kusema "Kanisa lao ndio mkombozi wa kweli wa Taifa na kwamba sala yao ni "very powerful prayer!" HAYO NI MAJIVUNO
Wee kina kuuma nini?.mbona na ww unasema kwako ndiko sahihi...so why uwapangie watu kujivunia kila wanachokiamini?.
Umepuyanga
 
Mbona nyie walokole mnasali kwa kupiga makelele na pia kutumia maspika makubwa, Hayo sio maombi ya kujionyesha?
Nikiandika kwa herufi ndogo hamuelewi? MAOMBI YOYOTE YA KUJIONESHA, MUNGU HAYASIKII, HAIJALISHI WANAOOMBA NI WALOKOLE AU WATU WA ILE DINI INAYOJIVUNA KUWA NDIO BABALAO
 
Back
Top Bottom