Habari za muda huu waungwana wa jamiiforums
Kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto hata mmoja, kunahitaji hekima na busara nyingi sana.
Hakuna ndoa yoyote hapa duniani ambayo ni rahisi kuipatanisha kwa maana kila ndoa ina changamoto zake, lakini ukweli wa mambo ni kwamba ndoa zisizo na watoto ni ngumu sana kuzipatanisha (kukitokea changamoto ya ziada) kuliko zile zenye watoto wengi au walau mtoto mmoja.
Kupatanisha ndoa iliyodumu kwa muda wa miaka 7 bila mtoto alafu iibuke changamoto nyingine mpya (ambayo inaweza kuwa ya kawaida katika ndoa zote hata zile zenye watoto) kama vile baba kuchelewa kurudi kazini, inahitaji hekima na busara ya hali ya juu sana.
Kwanini ninasema hekima kubwa inahitajika katika kupatanisha changamoto za ziada katika ndoa isiyo na watoto? Kwa utafiti mdogo nilioufanya kwa miaka kadhaa nyumba mpaka sasa nimegundua ya kwamba, ndugu na marafiki wengi wanaoitwa kwenda kusikiliza changamoto za ndoa yoyote ile, hukimbilia kwa watoto kama ngao ya kutaka baba na mama (wanandoa) wasitengane bali waendelee kuishi.
Hahahahaaaa unacheka? Unafikiri ninatania mkuu. This is very true my friend. Watu wengi wanaokwenda katika vikao hivi vya upatanishi hukimbilia kuwaambia wanandoa ya kwamba "Sasa
Infantry Soldier na
Bushmamy mkiachana leo hii, hawa watoto wenu watano wataishi vipi?"
"Sawa nyie watu wazima mnaweza mkawa na chuki zenu, lakini vp kuhusu future ya watoto jamani Soldier? Ina maana unataka kutengana na Bushmammy kisa tu chai ameiunga kwa nazi? Labda ndio mapishi yao huko Tanga mvumilie tu atabadilika taratibu" Hahahahaaaa, I'm joking, lakini bila shaka umepata mantiki yangu?
Watoto/Mtoto hutumiwa kama ngao ya kuzifanya ndoa nyingi ziendelee kuwa hai lakini licha ya ukweli kwamba baba na mama kila mmoja anakuwa analala chumba chake huko ndani au wanalala chumba kimoja lakini mwingine anatandika godoro chini.
Kama mtoto anatumika kama ngao kwenye ndoa zilizobahatika kupata walau mmoja, sasa zile ambazo zimekaa miaka 7 hazina kabisa unafanyaje kusuluhisha changamoto ya zaida inapojitokeza?
Ni ngumu sana ndugu zangu. Yaaani ni ngumu kweli kweli. Inahitaji watu wenye hekima na busara level ya ndugu zangu
Kiranga na
Mshana Jr ndio wanaoweza kunusuru ndoa za namna hii. vinginevyo labda Mungu pekee ndiye aingilie kati.
OMBI LANGU: Mungu tunakuomba uendelee kuwapa moyo wa uvumilivu na subira wanandoa wote ambao mpaka sasa hawajapata watoto/mtoto katika maisha yao na waamini ipo siku wewe kama muweza wa yote utawafungulia milango ya baraka na kuwapa hitaji hilo la mioyo yao kama ulivyomfanyia Sarah, mke wa Ibrahim. Amen.
Maoni ya wadau;
==========
==========
==========
==========
==========
USISAHAU:
ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.