Ulishawahi kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto/watoto? Hii inahitaji hekima na busara nyingi sana

Ulishawahi kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto/watoto? Hii inahitaji hekima na busara nyingi sana

Kinachowafanya Wapinzani waweseke ni Kwasababu Rais Samia ame wa outsmart kwa kila kitu.
 
Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, Yampongeza Rais Samia na Kuipongeza Tanzania, Kujenga Mazingira Bora ya Biashara ya Mafuta, Uwekezaji.
Long live samia Rais bora africa na dunia kwajumla.kwa kuishinda corona.
 

Habari za muda huu waungwana wa jamiiforums

Kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto hata mmoja, kunahitaji hekima na busara nyingi sana.

Hakuna ndoa yoyote hapa duniani ambayo ni rahisi kuipatanisha kwa maana kila ndoa ina changamoto zake, lakini ukweli wa mambo ni kwamba ndoa zisizo na watoto ni ngumu sana kuzipatanisha (kukitokea changamoto ya ziada) kuliko zile zenye watoto wengi au walau mtoto mmoja.

Kupatanisha ndoa iliyodumu kwa muda wa miaka 7 bila mtoto alafu iibuke changamoto nyingine mpya (ambayo inaweza kuwa ya kawaida katika ndoa zote hata zile zenye watoto) kama vile baba kuchelewa kurudi kazini, inahitaji hekima na busara ya hali ya juu sana.

Kwanini ninasema hekima kubwa inahitajika katika kupatanisha changamoto za ziada katika ndoa isiyo na watoto? Kwa utafiti mdogo nilioufanya kwa miaka kadhaa nyumba mpaka sasa nimegundua ya kwamba, ndugu na marafiki wengi wanaoitwa kwenda kusikiliza changamoto za ndoa yoyote ile, hukimbilia kwa watoto kama ngao ya kutaka baba na mama (wanandoa) wasitengane bali waendelee kuishi.

Hahahahaaaa unacheka? Unafikiri ninatania mkuu. This is very true my friend. Watu wengi wanaokwenda katika vikao hivi vya upatanishi hukimbilia kuwaambia wanandoa ya kwamba "Sasa Infantry Soldier na Bushmamy mkiachana leo hii, hawa watoto wenu watano wataishi vipi?"

"Sawa nyie watu wazima mnaweza mkawa na chuki zenu, lakini vp kuhusu future ya watoto jamani Soldier? Ina maana unataka kutengana na Bushmammy kisa tu chai ameiunga kwa nazi? Labda ndio mapishi yao huko Tanga mvumilie tu atabadilika taratibu" Hahahahaaaa, I'm joking, lakini bila shaka umepata mantiki yangu?

Watoto/Mtoto hutumiwa kama ngao ya kuzifanya ndoa nyingi ziendelee kuwa hai lakini licha ya ukweli kwamba baba na mama kila mmoja anakuwa analala chumba chake huko ndani au wanalala chumba kimoja lakini mwingine anatandika godoro chini.

Kama mtoto anatumika kama ngao kwenye ndoa zilizobahatika kupata walau mmoja, sasa zile ambazo zimekaa miaka 7 hazina kabisa unafanyaje kusuluhisha changamoto ya zaida inapojitokeza?

Ni ngumu sana ndugu zangu. Yaaani ni ngumu kweli kweli. Inahitaji watu wenye hekima na busara level ya ndugu zangu Kiranga na Mshana Jr ndio wanaoweza kunusuru ndoa za namna hii. vinginevyo labda Mungu pekee ndiye aingilie kati.

OMBI LANGU: Mungu tunakuomba uendelee kuwapa moyo wa uvumilivu na subira wanandoa wote ambao mpaka sasa hawajapata watoto/mtoto katika maisha yao na waamini ipo siku wewe kama muweza wa yote utawafungulia milango ya baraka na kuwapa hitaji hilo la mioyo yao kama ulivyomfanyia Sarah, mke wa Ibrahim. Amen.

Maoni ya wadau;
==========

==========

==========

==========

==========


USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kama ya kwangu bado ipo kwa sababu ya watoto tuu, bila hivyo kitamboooo.
 
Huwa nikiona hizi mada za kukosa watoto naumia Sana Kuna mama yangu mdogo(mke wa bamdogo) wamefunga ndoa mwaka 2006 mpaka Leo hajabahatika kua na mtoto wakati wa mwanzo wa ndoa alikua so charming na NI mrembo Sana,anakuja nyumbani kututembelea, tunaenda kwake kila mtu alikua anampenda yaani, kadri miaka ilivyokua inaenda akawa anabadilika Kuna function za familia akawa hashiriki Tena, akawa mtu wa hasira kipindi flani akajaribu kujiua bahati nzuri aliokolewa mwaka juzi mdogo wangu anayenifuata alipata mtoto nakumbuka wazo la kwanza akilini mwangu nilijiuliza sijui mamdogo alijisikaje aliposikia mwanaye amepata mtoto yeye bado maskini.
Huwa namuwazia Sana sijui kwanini.

Mungu awape kicheko wanawake wote mlioko kwenye ndoa na mnahangaika kutafuta watoto
 
mwaka juzi mdogo wangu anayenifuata alipata mtoto nakumbuka wazo la kwanza akilini mwangu nilijiuliza sijui mamdogo alijisikaje aliposikia mwanaye amepata mtoto yeye bado maskini.
Huyo mtoto aliyezaliwa, kama ni wa kike, alipaswa kupewa jina la bibi yake (ma' mdogo aliyekosa mtoto)
 
Huwa nikiona hizi mada za kukosa watoto naumia Sana Kuna mama yangu mdogo(mke wa bamdogo) wamefunga ndoa mwaka 2006 mpaka Leo hajabahatika kua na mtoto wakati wa mwanzo wa ndoa alikua so charming na NI mrembo Sana,anakuja nyumbani kututembelea,tunaenda kwake kila mtu alikua anampenda yaani,kadri miaka ilivyokua inaenda akawa anabadilika Kuna function za familia akawa hashiriki Tena, akawa mtu wa hasira kipindi flani akajaribu kujiua bahati nzuri aliokolewa
Duuuh kijiua tena? Inawezekana watu walikuwa wanamsimanga sana, tena ndugu wa mume.
 
Pole sana kaka mkubwa. Mbona sisi ambao hatujaoa mnatutisha hivi?
Hapana sisi wengine tuliangalia uzuri was mwanamke na mahaba yake kumbe hivo vitu havina dhamani kuleta furaha ya maisha katika ndoa.

Tuoliona kabisa hulka za ubinafsi, kisirani na gubu hatukujali tuliona kikubwa uko peke ako na kitandani fresh tukajua ndo mwisho...

Kumbe KABURI la kunizika mzima mzima
 
Hapana sisi wengine tuliangalia uzuri was mwanamke na mahaba yake kumbe hivo vitu havina dhamani kuleta furaha ya maisha katika ndoa.
Tuoliona kabisa hulka za ubinafsi, kisirani na gubu hatukujali tuliona kikubwa uko peke ako na kitandani fresh tukajua ndo mwisho...
Kumbe KABURI la kunizika mzima mzima
Mkuu, tumekutana tu humu JF lakini I can feel what you're going through. Pole kaka.
 
Back
Top Bottom