Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Waziri wa afya, inaweza kuwa uamuzi mzuri sana kwa serikali kuchangia na kulipa gharama za matibu kwa Joseph Haule.

Watu wana maswali sio juu ya ukarimu na utu wako katika maamuzi haya ila katika mustakabali wa afya za Watanzania kwa ujumla wake na ufikiwaji wa hii ya wizara yako kuamua nani anapata malipo ya bure na nani anapaswa kulipa

1. Umetumia kigezo gani katika kufikia maamuzi haya?
2. Je huu utakuwa mwendelezo kwa Watanzania wa aina gani?
3. Umefanya uchunguzi kidogo kuona namna ambavyo watanzania wengi hawawezi kumudu gharama za matibabu
4. Je wizara na serikali ina mpango wowote wa kuja na namna rahisi kwa watanzania kumudu gharama za matibabu?

Hongera kwa uamuzi wa busara na wenye kuonyesha huruma yako binafsi kwa Prof.J lakini umeacha maswali mengi.
 
Back
Top Bottom