Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naona unachanganya chuki na misimamo yangu. Tafuta popote ninapomtukana Mbowe, hadi useme nikiona anatukanwa napata faraja. Suala la Mimi kutokubaliana na kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya miaka 10 ni la principle zaidi. Kwenye hili sihitaji support ya yoyote, au kukubalika kwa yoyote.
 
..nilichogundua amekwenda Ccm kutafuta nafasi.
Hilo liko wazi, hata tone yake inadhibitisha hilo. Halafu ni kama anaghadhabu ya kutopata nafasi kwenye wale COVID-19.
 
Asingeweza; hakuwa na mamlaka hayo. Teknik ya hayati JPM ya kuufuta upinzani ilikuwa ni utendaji kazi uliotukuka, uliokuwa unapelekea wapinzani wahame wenyewe kutoka upinzani kurudi CCM
Katafute mjinga wa hivyo, ama unadhani hatukuona kipi kulikuwa kinaendelea kwenye ile hadaa ya kuunga mkono juhudi?
 
CHADEMA wavumilie kwasababu wao ndo wamemfundisha huyo Peneza matusi. CHADEMA ni chama kikuu cha matusi. Acha Peneza awape dawa.
Kwani ametukana wapi? Au kwakuwa kusema ukweli huko ccm kunachukuliwa kama matusi? Naona unalazimisha dhana zako kufit inn kwenye mahojiano ya Upendo.
 
Dada anafunguka vibaya huko clouds FM kuhusu mambo ya cdm. Anamuanika Mbowe hadharani.
Haya mambo ni ya kizamani mno. Haya mambo ya kutoka chama A na kukishambilia baada ya kutoka yalikuwa yanashangiliwa wakati wa ile miaka ya akina Mkapa. Mimi mtu hawezi kukaa kwenye chama kwa muda mrefu tu halafu atoke aanze kusema ubaya wa chama wakati muda wote alikuwa huko.
 
Kwanini Mbowe anakutumia sana kuliko sisi wewe chama, huoni uo ni ujuha, Mbowe washikilie hapo hapo,
 
Hongera unajitambua
 
Hawezi kuwa anaongea ya uongo yote. Suala la Mbowe na kina Mdee amesema kweli.
Hapa sasa.
Ningejuwa kaongea nini juu ya hili, nadharia yangu ingekamilika kabisa. Kwa bahati mbaya sipo karibu na 'CLOUDS' kwa sasa.

Ungetoa mstari mmoja tu, alichosema juu ya hili, ingesaidia sana mkuu 'Tindo'.

Mbowe alishafanya makubwa sana ndani ya CHADEMA, ambayo yangempa heshima kubwa katika historia ya chama hicho na Tanzania kwa ujumla.
Kuendelea kung'ang'ania kuwa kiongozi wakati huu, kutamwondolea sifa zote, na huenda akakiua chama chenyewe.
 
Uzi umeenda mbali huu, kuna post yangu humu humu nimeweka alichosema kuhusu hilo. Ila anaonyesha shaka ya dhahiri kuhusu Mbowe na Mdee Hadi kufikia kualikana binafsi kwenye sherehe, na michango madhabahuni. Kikubwa ni mwenendo wa cdm kwenye kesi ya hao COVID 19.
 
Nautafuta "mchango huo."
Lakini usisahau pia kutapatapa kwa CCM wakati huu tukielekea chaguzi muhimu. Watatumia kila uchafu; hata kuua wakiweza, ili waendelee kutuweka mateka wao.
 
Amesema kuhusu pesa walizokuwa wanachangishwa wao kama wabunge, hawafahamu zimetumika kufanya Nini. Na ni kweli hizi pesa zimekuwa zikitolewa porojo. Huyu Upendo kwakuwa ana hasira ataongea mengi ya hasira, lakini humo ndani tutapata ukweli.
Aangalie hasira zisije zikamuharibia future yake. Sijamsikiliza kwa kweli ila sijui kama alishawahi kuuliza kwenye vikao vyao kwa kuwa nae alikuwa kiongozi mkubwa tu. Au kwa sababu alkkuwa ndani aliogopa kutingisha ndevu za boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…