Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
kwani nani amekwambia hawatalazimishwa?

Kwani wapi nimeandika hawatalazimishwa ndugu?

Au hata wapi nimesema miye ni nabii hata nikathubutu kuyaongelea ya kesho?
 
Bibie wa Unguja alimpongeza Putin haraka haraka na sote tunajua kuwa kulikuwa uwizi mkubwa wa kura kwenye Uchaguzi wa Russia.

Sasa ngoja tuone kama atampogeza Faye wa SenegalπŸ‡ΈπŸ‡³ mshindi halali.

Vipi angali kauchuna?

 

Tofautisha marais na wale wengine:

 
Hapa kwetu cdm walikuwa wanaenda vizuri Hadi walipojichanganya na kuokoto jizee toka huko ccm. Na Sasa naona wanaendelea tena kupotea maboya kwa kukubali maridhiano fake. Haitakiwi porojo za maridhiano, Wala kushiriki chaguzi kwa katiba hii hii ya hovyo na tume ya uchaguzi ya kihuni. Msimamo ulitakiwa ni mmoja, hakuna katiba mpya, hakuna kushiriki upuuzi uitwao uchaguzi. Watu wanajali uhai wa vyama kwa fedha za vijirizuku uchwara

Kitendo Cha kuuharamisha uchaguzi ni mwanzo wa kuelekea kwenye madai ya haki, kwani uchaguzi huo utakuwa na wapiga kura wachache mno. Kutoka hapo automatically itengenezwe movement ya kudai katiba mpya kwa namna yoyote ile, hata kwa machafuko au mapinduzi ya kijeshi.
 
Ndio, katika Biblia, HAKUNA MAMLAKA ITAKAYODUMU milele, tujitayarishe kisaikolojia....
 

Msimamo ulitakiwa ni mmoja, hakuna katiba mpya, hakuna kushiriki upuuzi uitwao uchaguzi.

"Watu wanajali uhai wa vyama kwa fedha za vijirizuku uchwara."

Ruzuku zifutwe. Ruzuku ndizo zinazotugharimu.
 
Yale yale ya Tundu Lissu vs Mtu yule
 
Msimamo ulitakiwa ni mmoja, hakuna katiba mpya, hakuna kushiriki upuuzi uitwao uchaguzi.

"Watu wanajali uhai wa vyama kwa fedha za vijirizuku uchwara."

Ruzuku zifutwe. Ruzuku ndizo zinazotugharimu.
Kabisa, msimamo ni mmoja, wananchi hakuna kuendelea kujitokeza kushiriki chaguzi za kuhuni hata kama vyama vyote vitaendelea kushiriki huo uhuni. Hiki kitendo Cha kuendelea kushiriki uhuni huku wengine wanapora uchaguzi, wengine wanaishia kulalamika kuibiwa kura na hujuma za wazi kwenye uchaguzi, wananchi tunapoendelea kushiriki chaguzi za hivyo inaonekana tumeridhika na huo uhuni.

Cha muhimu ni kutojitokeza kwa wingi kupiga kura, na kiongozi atakayeshinda kwenye hizo chaguzi za kihuni hakuna kumpa ushirikiano. Akiitisha mkutano hakuna kujitokeza, akihoji watu kutojitokeza aambiwe kabisa Hana uhalali wa umma. Hapa hata ikitengenezwa movement dhidi ya utawala usio na uhalali wa umma itapata nguvu.
 

Ni vyema viongozi wetu wakajua wanao wajibu wa kutusikiliza.

Wao si miungu watu. Demokrasia ni kuwapa yao walio wengi.

Itambulike kutofautiana kimawazo ni jambo la afya tu wala si usaliti.
 
Watz wengi wetu hatujiekewi mpaka hao wapinzani wenyewe, sahau hii kutokea nchi hii. Kama makonda tu anakuja na guta kwenye mkutano kisha tunapiga vigelegele na kumuita mbunifu huku tukikenua meno yote unategemea nini. Kichwa cha mwenda wazimu.
 
Upinzani haijawahi kuwa ishu huko ,hata Rais anayemaliza mda wake alikuwa mpinzani na akataka kung'ang'ania madaraka πŸ˜†πŸ˜†

Swali la msingi ni baada ya hao Wapinzani kushika Dola nini imekuwa Tija Kwa wale waliowapigia kura na kushangilia na wengine kuuwawa mitaani?

Ni ujinga kuacha kazi zako ukatumikishwe na Wanasiasa kama hunufaiki na chochote.
 
Watz wengi wetu hatujiekewi mpaka hao wapinzani wenyewe, sahau hii kutokea nchi hii. Kama makonda tu anakuja na guta kwenye mkutano kisha tunapiga vigelegele na kumuita mbunifu huku tukikenua meno yote unategemea nini. Kichwa cha mwenda wazimu.

Tatizo kubwa kutojulikana falsafa za vyama:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

Haieleweki vyama vinapigania nini.

Wajielewe vipi kwenye mazingira ya sasa?
 
Ni vyema viongozi wetu wakajua wanao wajibu wa kutusikiliza.

Wao si miungu watu. Demokrasia ni kuwapa yao waluo wengi.

Itambulike kutofautiana kimawazo ni jambo la afya tu wala si usaliti.
Kiongozi akilazimisha kushiriki uchaguzi wa kihuni unampotezea, akipeleka chama kushiriki uhuni kwa ahadi za uchochoroni , atakuta wapiga kura wachache, ndio atajua watu hawataki upuuzi tena. Ifahamike nguvu ni za wananchi sio viongozi.
 

Tambua sababu za mapambano:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

Kama wewe ni mjasiliasiasa huku hakukufai.
 
Tatizo la tanzania rais anateua watu weni mno ambao hubadilika kutetea mamlaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…