Ushoga na usagaji changamoto zinazowatesa wengi kimyakimya kwenye familia na kwenye ndoa

Ushoga na usagaji changamoto zinazowatesa wengi kimyakimya kwenye familia na kwenye ndoa

Wazazi kuweni makini sana, halafu watoto wenu wapeni sifa zao kama ni wa kike, afanye ya kike, wa kiume ndio kabisaa...

Kuna mdada tumezoeana sana, ni mtu wangu wa karibu mnoo,
Siku moja nimefika pale kwa mualiko wa msosi wa mchana,
Akanipa kesi, kuwa mwanae wa miaka mi4 kwamba jana karudi wakati anamuogesha kamuona ana mafuta kwenye kiuno karibia na tako, kumuhoji, akasema shuleni kuna mtoto mwenzake huwa anakuja na mafuta, ukizubaa anakupaka.
Nikamuuliza unavyoona hajaingiliwa akasema hajaingiliwa,umechukua hatua gani !?
Akasema kamchapa, akiona kapakwa mafuta tena atamchoma moto, nikamwambia umejitahidi ila kwangu naona bado,
Kwanza nenda ukaripoti shule ili uwe msaada kwa watoto wa kiume,
Pili mlete uncle niongee nae, akaja tukapiga stori, ikawa kila nikienda tunapiga stori namjaza sumu zangu.
Siku ya siku yule dada akanipogia simu anacheka kweli, namuuliza vipi, ananiambia anamuona mwanae kabadilika, kwanza ni anapenda sana tamthilia za ngumi, zile za kituruki, yaani wao wakiangalia zile za mapenzi hana mpango anasubiri za mapanga sha..
Kingine akasema juzi kati ameanza tabia akiwa anamuogesha akitaka kumgusa makalio katika kumuogesha, anamkataza, anamwambia uncle kaniambia mwanaume haguswi makalio na mtu yoyote zaidi ya yeye mwenyewe, anataka ajisafishe mwenyewe makalio, siku hizi hata akijisaidi kumchambisha ni mbinde.. 😂😂
Nikamwambia dawa imemuingia, sasa ndio amlee kiume sio kimama mama.
Hahaha😂😂😂 ila hapo kwenye ukaribu nadhani kuna la ziada
 
Hahaha😂😂😂 ila hapo kwenye ukaribu nadhani kuna la ziada
Hapana, ni ukaribu wa kawaida, si unajua sisi watoto wa mjini, akihitaji fundi umeme mie ninae ambae tena atafanya kazi kwa bei rafiki tofauti na huko nyuma alivyoluwa akipigwa, akitaka fundi ujenzi ninae, akitaka simu nzuri na kali anapata ushauri na wapi itapatikana kwa bei rafiki... Si inajua watoto wa mjini tunajua mengi mengi .

Kati yetu kuna utofauti wa takribani miaka 20 hivi
 
Umemtafuna mama yake 😹😹
Sema umejua kulipa fadhila kwa kumsaidia kijana wake, na mimi nitakualika nikipata mtoto..!! 🤣
 
Tatizo hili namba moja linachangiwa na.
1.Single Parenting- Single parenting hii kitu inamchango mkubwa sana sababu chuma hunoa chuma,yaani baba ndiye role model wa kwanza kwa mtoto wa kiume na hivyo hivyo kwa mto wa kike role model ni bi mkubwa wake,ila ndio hivyo hizi single parenting zina mchango mkubwa kwenye hili tatizo. Kuna wanawake waamaini pesa zao zinaweza kulea mtoto (wasomi na wanaharakati/feminis, kuna wanaume nao sababu bi wakubwa wao akizinguana na binti anampeleka kwa bibi yake then yy anafanya mambo yake,kwani hawajui hela hailei mtoto bali inamtunza mtoto.

2.Malezi- Siku hizi wengi wanazaa ila hawajui kulea wala kufuatilia watoto wao,wao wanakimbizana na hela wanaondoka saa kumi na mbili jioni, kurudi saa nne usiku mda huo watoto wamelala, hana mda wakumfuatilia mtoto issue ya malezi,hajui mtoto anapokuwa home anatizama vitu gani kwenye TV,kampani anayo tembea nayo hajui, hajui kwa siku anapotoka na kurudi shuleni anakutana na chamoto gani kamwachia house girl/boy.Sasa bora upate homeboy/girl mwenye tabia nzuri kiroho kwani wapo wachache.Mzazi kazi yake ni kulipa ada na hela ya kula kwa kifupi wanatunza badala ya kulea. Huwaga na wambiaga mabinti wajitahidi katika siku za wiki basi hata tatu,wajitahidi kuwa karibu na watoto hasa wakati wa kuwaogesha, wajaribu kupiga nao story,mara nyingi watoto kipindi kile huwa wanafunguka vitu vingi japo sometimes huwaga vya kitoto,ila kuna moja litakusaidia kung'amua directions ya mwanao.

3.Mazingira-Kuanzia mtaani huko mpaka shuleni,siku hizi mitaani huko kuna matarumbeta na vigoma vinakusanya mapunga kibao, wakiwa wamevalia nguo za kike, ile ni hatari sana kwa mtoto wa kiume anayekua akiona vitu hivyo. Bila kusahau shule kuna shule za bording nyingine zinafahamika kwa kukoboana na kulana ndogo,kuna mwamba mmoja ana hela ila kasema mwanae hatosoma shule ya boys,atampeleka shule za mchanganyiko kuanzia primary mpaka secondary nk,kasema mwane hatosoma shule ya jinsia moja.

4.Tamaa- Vijana siku hizi wanatamaa kuna wanawake matomboy wanahela nao wanajua kuitumia hii silaha kwa wanawake. Kuna mabasha wanawashawihi vijana wenye tamaa na wamewaweka ndani na kuwapatia kila kitu kama wake zao, kuna mapunga tena hawa ndio wanakuja kwa kasi nao wanatumia pesa kupata mabwana ambao watawasugua na wanathubutu kukaa nyumbaa moja kama mme na mke. Vijana wa siku hizi huvumilivu hawana hata kidogo na hii huchangiwa na hizi Social networks. Wakiwaona watu kwenye social networks wanalingishia magari,nyumba kali simu wanahisi wamechelewa sana,kumbe asilimia zaidi ya tisini ni maigizo vitu si vyao. Kichwani mwake anajaa taama na kujiambia atafanya lolote ili na yy apate hivyo vitu.

5.Mitandao ya ngono, movie, majarida haya- Miaka ya nyuma denda lilikuwa kitu cha ajabu na kumbuka sometimes, huwaga ikifikia hilo eneo hubadilisha channel kwa dk kadhaa,ikaja kwenye scene za kupigana miti kwenye movie na hivyo hivyo hubadilisha channel au hupeleka mbele ili hiyo sehemu ipite ili siku hizi ni kama kawaida kwenye movie kulana denda na kupigana miti. Siku hizi series nyingi mpya za miaka kuanzia 2010+ zina part ya maswala ya upinde, kwenye mitandao huko ndio wamejiachia kuna mazingira fulani yanajengwa ionekane ni kitu cha kawaida,sometimes waarabu na waelewa wanapo control baadhi ya maadhui na hata baadhi ya mitandao ya jamii hasa tiktok.

Cha msingi kama mzazi timiza wajibu wako kwenye kulea na kumfuatilia mwanao, husimwache mwanao alelewe na watu baki au ndugu, sawa tunatafuta hela ila hela zitakuwa hazina maana kama ukiona mwanao anatabia hizo. Vijana punguzeni tamaa ,rahisisha mahitaji yako ,huku ukifanya kazi kwa bidii kuna siku utapata kile ulicho kitamani kupitia jasho lako.Mtangulize Mungu na kumshirikisha Mungu kwenye malezi ,makuzi na utafutaji wako na Mungu atakusikia.
 
Hapana, ni ukaribu wa kawaida, si unajua sisi watoto wa mjini, akihitaji fundi umeme mie ninae ambae tena atafanya kazi kwa bei rafiki tofauti na huko nyuma alivyoluwa akipigwa, akitaka fundi ujenzi ninae, akitaka simu nzuri na kali anapata ushauri na wapi itapatikana kwa bei rafiki... Si inajua watoto wa mjini tunajua mengi mengi .

Kati yetu kuna utofauti wa takribani miaka 20 hivi
Na siku akihitaji? 😀 miaka sio hoja huo wema anaweza kuuvisha koti la kuvutia
 
Umemtafuna mama yake 😹😹
Sema umejua kulipa fadhila kwa kumsaidia kijana wake, na mimi nitakualika nikipata mtoto..!! 🤣
Hahaa.. hapana, haipo hivyo ni mshikaji tu, kati yetu kuna gap kubwa tu la umri, yule hamna hamna kwenye 50+ ama 47,49 hivi.

Nausubiri huo mualiko,sauti yako ile jana inafaa kwa matumizi ya KIBAYOLOJIA 😂🤣
 
Back
Top Bottom