Usitafute utajiri, utajiri ni matokeo. Tafuta kibali cha Mungu

Usitafute utajiri, utajiri ni matokeo. Tafuta kibali cha Mungu

Roho za umimi hizi. Tafuta mali vizazi vyako vije viishi vizuri. Hapa ndipo wanapotushindia wazungu
Kama ni hivyo basi nimeisha watafutia wanangu
Mpaka wa miaka 10 ana nyumba yake tayari ila itakuwa yake mda ukifika
Na hajui ila ipo kwenye WILL
Ila ukweli utabaki pale pale ntaondoka mimi kama mimi hayo yanayobaki hayahesabiki kama yangu tena
Hata uwe mfalme ila utaondoka masikini tu na mali zako watabaki nazo wengine

Hili la kuondoka mtupu ni lazima halina mjadala au ni mawazo ya umimi
By the way niko kwa wazungu na hawaachiani mali kama hujazitolea jasho

Usiwasifie niko nao miaka 35 leo
 
Kwenye maisha kuna Bahati (Luck) ambapo binadamu yeyote anaweza kuipata pasipo kutarajia.

Na bahati hii, Haina uhusiano wowote na nguvu za kiroho kwa sababu huweza kumtokea mtu yeyote.

Wateja kuja sana kwenye biashara yako si kwamba eti una kibali na si kwamba wewe pekee ndio una wateja wengi hapo mtaani kwako au kwenye biashara yako.

Wateja kuwepo kwa wingi kwa mfanyabiashara fulani, inategemea na vitu vingi sana kama kauli nzuri kwa wateja, ubora wa bidhaa zako, namna unavyo toa huduma, muda wa biashara yako ulipo ianza na uzoefu wako wa kujuana na wateja n.k

Hapa hakuna kibali wala nguvu yeyote ile.

Kama unabisha, Jaribu kwenda kinyume na kanuni hizo uwe na kauli mbaya kwa wateja, utoe huduma mbovu, uza bidhaa zisizo na ubora tuone kama hicho Kibali chako kitafanya kazi.

Point yangu ni kwamba, HAKUNA uhusiano wa kibali na mafanikio ya mtu kwenye nyanja za kimaisha.

Kibali ni dhana ya kufikirika. Haipo.
Unakataa Mungu hayupo ila unakubali uwepo wa bahati, na huwa unakaza fuvu kabisa wewe ni Mwanasayansi unaeelezaga vitu kwa empirical evidence?

Dunia simama nishuke [emoji1732][emoji1787]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ni ngumu kukupa chakula cha kiroho na ukaelewa kwa maana humuamini mtoa hcho cha kiroho hvyo itakuwia ugumu sana katika kuelewa nin maana ya hcho #KIBALI.

Pili kuhusu kuomba na kupewa baraka na mahitaji yako kwa muumba wako ni lazma umuombe kwa maana unapo muomba ndo unadumisha utukufu wake kwa kumnyenyekea, ndivyo apendavyo kwa maana yey n mkuu na ndo muhimili juu ya vilivyo hai na vilivyokufa.

Ni mfano mdogo tu, hv ulishawah kwenda dukani kwa mangi na noti ya elfu kumi ukakaa kmya tu bla kuzngumza chochote na mangi akajua na kukupa mahitaji yako??

Na kwanin mung akupe mahitaj yako bila kuonesha nia ya uhitaji?? Hapo ndpo linapokuja suala la kuomba kibali

Ila itakuwia ugum kuelewa kwa maaana uamin katika mungu na tayar umeandaa majib yako, ambyo n kinyume cha uzi na mada tajwa hapo juu.

Mungu Yupo na miujiza yake ipo wazi, muda bado unao. Usije ukajua umuhimu wake wakat upo nje ya mda.

#Amiin[emoji1621][emoji1621]
Ni vigumu sana kumuelimisha Mtu aliyejiandaa kiakili kubisha, unaweza ukapatwa na njaa usiyotarajia...[emoji142]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Unakataa Mungu hayupo ila unakubali uwepo wa bahati, na huwa unakaza fuvu kabisa wewe ni Mwanasayansi unaeelezaga vitu kwa empirical evidence?

Dunia simama nishuke [emoji1732][emoji1787]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Bahati ina thibitisha vipi uwepo wa Mungu?

Una elewa maana ya bahati?

Bahati ni jambo linalo tokea pasipo wewe kutarajia, Wala halioneshi uwepo wa Mungu.

Ushuke sasa duniani umefika.
 
Nikiyajua mahitaji yao siwezi kusubiri waombe. Yale nisiyoyajua nitasubiri waombe.

Natumai Mungu yuko hivyo pia kama Mimi, au?
Ndio haswa.. Pumzi huiombi anakupa, uhai huombi anakupa nk
 
Roho za umimi hizi. Tafuta mali vizazi vyako vije viishi vizuri. Hapa ndipo wanapotushindia wazungu
Thibitisha kuwa na mali ndiyo sababu ya kuishi vizuri.

Wangapi mali zimewakatisha uhai kabla ya siku zao?

Je athari za dhuluma za mirathi ya mali kwa Watoto baada ya mwenye mali kufariki ikiwemo hata wao kutishiwa maisha?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ndio haswa.. Pumzi huiombi anakupa, uhai huombi anakupa nk
Ni vipi siombi wakati uhai wangu unategemea jitihada zangu? Aje kama nikibweteka nisile, je sitakufa? Aje kama nitakunywa sumu au kujinyonga? Ananipaje uhai mimi pasi mimi kuuomba?

Natafuta sehemu salama, chakula salama, mahusiano salama, mazingira salama, nk ili niishi, UNASEMAJE KUWA HIZO SI JITIHADA ZANGU?
 
Mungu mwenye upendo, Na angekuwa Anatupenda.

Je angeruhusu uovu, dhambi, mateso, ukatili na ubaya, Viwepo Duniani?

Mungu huyo ana tupenda kweli?

Mungu mwenye upendo, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Uovu wala ubaya wa aina yeyote ile?

Mungu mwenye upendo, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kutenda dhambi na mabaya?

Huyo Mungu anatupenda kweli?
'MUNGU amemfanya mwadamu mnyoofu lakini wamebuni mavumbuzi mengi'
Ni vipi siombi wakati uhai wangu unategemea jitihada zangu? Aje kama nikibweteka nisile, je sitakufa? Aje kama nitakunywa sumu au kujinyonga? Ananipaje uhai mimi pasi mimi kuuomba?

Natafuta sehemu salama, chakula salama, mahusiano salama, mazingira salama, nk ili niishi, UNASEMAJE KUWA HIZO SI JITIHADA ZANGU?
Unafanya jitihadi za kuutunza lakini huna mamlaka ya kujiwekea ama kuuondoa uhai.. kabla sijaendlea ningependa kujua Kama unaamini MUNGU yupo au la?
 
Mabaya, maovu, magonjwa na mateso kuna ambaye Huomba Mungu awenayo?

Je na haya Mungu anatoa sio?
Yeah Kuna scenario zipo anatoa yeye kwa makusudi yake kwako either akukomboe mwishoni , Ila mengi ya hayo hutoka kwa kwa yule 'MWOVU'
 
Thibitisha uwepo wa bahati physically and its visibility.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Bahati hutokea katika mazingira ya kuonekana.Na si katika mazingira yasiyo onekana.

Bahati haina uhusiano wowote ule na nguvu za kiroho zisizo kuwepo.

Labda nikupe, mifano.

Mtu kubashiri mechi (kubeti) na kushinda ni jambo la bahati na si kwamba jambo hilo haliwezekani au jambo hilo lina uhusiano na nguvu yeyote ile ya kiroho,

Ni bahati ya mtu tu, Ndio maana wapo wanao bahatika kushinda mamilioni, Lakini si watu wote hubahatika kushinda mamilioni hayo. Hii ni bahati tu katika mazingira yanayo onekana.

Wakati mwingine bahati hutokea katika mazingira ya Usahaulifu, Mfano Kuna matukio mbalimbali ya miamala ya kifedha kutumwa kwa watu wasio sahihi. Watu hawa wanao pokea fedha hizi huona kama ni bahati hivi imekuja kwao. Lakini ni bahati katika mazingira ya Usahaulifu.

Wakati mwingine bahati huja kutokana na mtu kupendezwa na mtu fulani, Mfano Mtoto wa jirani amefaulu vizuri kimasomo na akabahatika kupata mfadhili wa masomo yake, Hapa "bahati" imekuja kutokana na juhudi za mtu binafsi zilizo pelekea mtu kupendezwa na juhudi hizo. Wala hakuna mazingira ya kuonesha uhusiano wowote wa bahati hii na nguvu za kiroho.

Wakati mwingine bahati hutokea katika mazingira ya uzembe wa kibinadamu, Ambapo mtu mwingine hudhani ni bahati kwake, Mfano Ajali ya Magari ya cement au mafuta inapotokea wale wanao enda kugombania cement au mafuta hayo hudhani na kuona kwamba ni bahati kwao ajali hiyo kutokea ili wao wapate, kumbe ni uzembe wa kibinadamu tu uliyo sababisha ajali na kupelekea bahati ya wakazi wa eneo hilo kupata cement na mafuta.

Pointi hapa ni kwamba "Bahati" Haina uhusiano wowote ule wa uwepo wa nguvu za kiroho na uwepo wa Mungu.
 
Back
Top Bottom