Utabiri: Mwaka huu hautaisha kabla ya Dola ya Marekani kufika 3000Tsh

Madhara makubwa ya vita ya Ukraine VS Urusi,Middle East instability imefanya uchumi wa dunia uyumbe zaidi..

Nchi zijazoendelea zinapaswa kuchukua hatua Za makusudi kujenga uchumi imara wa ndani usioegemea Kwenye Importation and trading..

Tufanye uzalishaji mkubwa wa ndani..Tupunguze uagizaji unaogharimu mabilioni ya dola kila mwaka..

Tupunguze matumizi yasio ya lazima..Tusimamishe miradi mikubwa..Uwekezaji kwenye kilimo uongezeke
 

Hii ni kuuza dola

Kununua dola now 2800
 
Magufuli ndiye alituletea Samia, kama sio magufuli tusingekua na rais kama samia. Alaumiwe magufuli kwa hili balaa

Chaguo lake lilikuwa ni mwinyi. Ila ngosha ni ngosha. Second term he was supposed kuwa na makamu mwingine

Ishu ya uzanzibar kuwa makamu ilichangia ili kubalance muungano. Ila hiz habari za kubalance muungano some days zitatucost snaa

All in all mama anaupiga mwingi all the best my Samia
 

Tatizo kubwa ni wasomi kama nyie ni wasomi wa nyuma ya keyboard, mtu kama lissu mnaona anataka kuvuruga aman

Hakuna
Nchi iliyoendelea kwa wasomi kujificha nyuma ya keyboard kama wewe kaka
 
Hilo suala wala hata huhitaji utabiri. Liko obvious sana.
Ni sawa na kusema mwaka huu mpaka unaisha bei ya Petrol haitakua chini ya 3,500.
Mbona trend zinaonyesha dhahir shair bila kuficha
 
Tunaotuma pesa mtandaoni iko $1 = TShs 2,858
 
Pesa ya Zimbabwe (ZWL) iliwahi kushuka mpaka mtu unaenda sokoni na tololi la minoti eti tololi zima kwa kuchenge to Tz ni shilling 40000.
Wakaona ni ujinga walicho fanya wanatumia USD doral kama pesa ya taifa.
Mkuu naomba unieleweshe kama sisi tukifanya hivyo madhara yake ni nini? Yaani kwamba tuondoe madafu kwenye mzunguko halafu ibaki $ inatamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…