Ukiwa na hofu ya Mungu utapata hekima, sio binti. Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa. Nje ya hapo ni maneno ya kutoka kwa yule mwovu. Kumbe hekima ya KUMTOA BINTI AOLEWE haina jipya zaidi ya hekima ya Mungu. Tabia mbovu ya wazazi wa kisasa; wanawake ambao binti zao katika ukahaba kisha wanakuwa na mashaka kama watabaki salama kwa waume zao. Ndivyo pia wanavyolelewa vijana wa kisasa, hawajui hata majukumu ya ndoa. Matokeo yake ndoa imegeuka taasisi ya majaribio. HEKIMA INA MUNGU PEKEE.
Kwa ndoa za kisasa wazazi tumechangia sana kufanya institution ya ndoa kuwa useless si mabinti wala vijana wa kisasa wanajua maana ya ndoa zaidi ya kufanya harusi kubwa.
Binti wa kisasa anafundishwa kujihami kwa mwanaume kwa kuwa mama na bibi zake walinyanyasika, kijana wa kisasa bado anaandaliwa kizamani kuwa wanawake ni watulivu na wavumilivu kumbe sio hawa wa kizazi kipya ni balaa tupu.
Kwa majirani hapo Kuna wimbi la wanaume kuuwawa naona ndio tunakoelekea huko.