UTEUZI: Amos Makalla ahamishiwa Mwanza, Chalamila apelekwa Dar
Makalla ni CPA Hakuna mtu mwenye sifa ya kutatua migogoro ya kibiashara hasa kuhusu kodi kama mtu mwenye hiyo qualification.

Tells you hawa watu hizi qualifications zao wanavyozipata kwa kuunga unga, yeye kwa elimu yake aitakiwa kulimudu hilo swala ana uwezo wa kuwa challenge both TRA na wafanyabiashara kupata muafaka; kushinda huyo waziri mkuu.

Hakutosha kwa mkoa wa Dar kwa jinsi alivyo deal na hilo sakata la kodi kwa qualification zake.
 
Chalamila Dar??🤣🤣🤣🤣

Huu ni uchonganishi wa kumuondoa kabisa. Dar inahitaji mtu aidha mkorofi kama Makonda au mwenye hekma kama Mecky Sadick
Makonda alikuwa na ukorofi gani .yule alikuwa mpumbavu mara shisha mara ushoga .dar kairudisha nyuma sana
 
Huyo mtaka aliyekamata mtu aliyebambikiwa maparachichi machanga!! Na kumfanya Mhalifu badala ya kumsaidia kutafuta waliomuingiza Chaka!! Hakika Jiji la Dar hataliweza!! Uwezo wake unatia Mashaka
Hawezi. Pia sio mfuata sheria huwa anajiamulia tu mambo yake. Alishawahi kukwaruzana na waziri wa elimu kuhusu kambi za vijana za kujisomea. Lile lilikuwa ni doa kubwa sana.
 
Wakuu wa mikoa wanakazi gani kama sio kubebana na kula pesa tu
Screenshot_20230516-004625_WPS Office.jpg
 
Nini maana ya kumhamishia mkoa mwingine, hawezi kuongoza, hatatui migogoro ama ni usanii huwa unafanyika?!
 
Mtu mwenye ubobezi kwenye mambo ya Uchumi, mtu mwenye vitufe vya vyombo kama TISS uchumi, unashindwa vipi kudadavua na hata kuepusha suala linalowoweza kupata kioo (spotlight: if you may)kwenye vyombo vya habari vya "Wawekezaji" ? Inaleta taswira gani kuhusu hali ya usalama, kwa wananchi na wafanyabiashara, wanunuzi n.k .nk na Upande wa kiserikali, Intelligence services za Mkoa ukiachilia mbali za Nchi. Kha!

My teke, ndio my teke RC Makalla kama kada na mbobezi wa mambo ya Kisiasa-amefail Kama mbobezi wa mambo ya Kiuchumi-amefail. Kama kiongozi wa Mkoa mkubwa Nchini amefail kuyaona, kuepusha, na ninavyofikiri, kuchelewa kupeleka ripoti ya uzito wa (impact analysis)yaliyokuwa yatafanyika,(an apparent mgomo)/kwa uzito uliohitajika na kwa wakati muafaka. Nafikiri hili jambo hakulipea maani na uzito unaotakikana kupewa kwa Mkuu wa Mkoa mwenye Ubobezi kwenye masuala ya Kiuchumi, Kisiasa na Kiusalama ukizingatia umuhimu wa Mji kama Dar na uchumi wake kwa Ujumla. In short amefail. Hayo mengine yakuzungushwa zungushwa...have at it.

"Not a time to be wobbly" the Irone lady once said.
 
Back
Top Bottom