UTEUZI: Amos Makalla ahamishiwa Mwanza, Chalamila apelekwa Dar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.
View attachment 2623197

KUHUSU MAKALLA

Makalla alishawahi kushika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa CCM na aliwahi kukaimu nafasi ya katibu wa umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM).

Pia. Amewahi kuwa mbunge wa Mvomero kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho alikuwa mbunge mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Makalla pia, amewahi kuwa naibu waziri wa habari enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kisha kuhamishiwa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Katavi.

Mei 14, 2019 Hayati John Magufuli alitengua uteuzi wake akiwa mkoani Katavi.

Mei 15, 2021, Rais Samia alimteua Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam

Pia, soma: Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam
Kusema ukweli Makala hafai kuwa kiongozi,sema ndo hivyo tena.JK alimuomba Samia amteue.
 
Hakuna mkoa ambao makala atafanikiwa . Amejaa Blaablaaa
 
Dar angeweza sana Anthony Mtaka au Gabriel yule alikuwa RC Geita zamani, Chalamila hapana kabisa, ngoja tuone
 
Back
Top Bottom