UTEUZI: Amos Makalla ahamishiwa Mwanza, Chalamila apelekwa Dar
Huyo alibebwa na Kikwete baadae akabebwa na Magufuli nae akaona mzigo akamtupa mama kaja kamuokota analazimisha ila huyo ndio anaondoka hivo!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.
View attachment 2623197

KUHUSU MAKALLA

Makalla alishawahi kushika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa CCM na aliwahi kukaimu nafasi ya katibu wa umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM).

Pia. Amewahi kuwa mbunge wa Mvomero kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho alikuwa mbunge mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Makalla pia, amewahi kuwa naibu waziri wa habari enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kisha kuhamishiwa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Katavi.

Mei 14, 2019 Hayati John Magufuli alitengua uteuzi wake akiwa mkoani Katavi.

Mei 15, 2021, Rais Samia alimteua Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam

Pia, soma: Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam
Amos Makala na Chalamila ndio wakuu wa Mikoa pekee waliwahi kuongoza Mikoa mikubwa ya Tanzania Kwa manaa ya Mikoa yenye uchumi mkubwa ambayo ni

Dar,
Mwanza
Mbeya
Screenshot_20221025-203055.png
 
....anakujaje huku kwa daslama...
Nikiangalia ID yako hapa JF, nakuona kama verified user!
===
Maamuzi ya kumleta Chalamila Dar es Salaam yamefanywa na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Kuijadili uteuzi wake kwa lugha hizi za kuudhi hakukubaliki. Kwa jeuri yako unaweza usiombe radhi. Lakini, nakushauri ujifunze kuwa na staha.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.
View attachment 2623197

KUHUSU MAKALLA

Makalla alishawahi kushika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa CCM na aliwahi kukaimu nafasi ya katibu wa umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM).

Pia. Amewahi kuwa mbunge wa Mvomero kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho alikuwa mbunge mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Makalla pia, amewahi kuwa naibu waziri wa habari enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kisha kuhamishiwa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Katavi.

Mei 14, 2019 Hayati John Magufuli alitengua uteuzi wake akiwa mkoani Katavi.

Mei 15, 2021, Rais Samia alimteua Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam

Pia, soma: Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam
Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Maji.... Siyo Naibu Waziri wa Habari... Rekebisha hapo!

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom