Asanteni sana @tanpol !!! Tunawapenda SANA!! SISI ni watu wema!!! Tanzania ni YETU SOTE. Tusiruhusu maslahi ya WATU wachache watuvurugie UPENDO wa ASILI wa TAIFA LETU-Halima Mdee

Halima amefanya vyema, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali kuchukua maamuzi hasi.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano huu rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi.
 
 
Anashiriki kutekeleza wajibu wake Wa Kibinadamu.. Watakaochukia yeye kushiriki msiba wana matatizo yao
 
Nakwambia hivi mwenyewe sikutegemea lissu atapona kwa hali ile, ingawa kabaki na makovu, viraka, dah inauma sana

Mungu unae muomba lissu tunaomba utwambie na ss tumuombe anaweza jibu maombi yetu mapema sana,

Akiwa raisi wasio julikana watapakina ata kuzimu watafufuliwa warudiashwe Tanzania
 
Hapana Yule alikuwa Raisi wetu, Lazima twende kumuaga.
 
Makonda mpeni kazi ya kutotoresha mayai ya tausi msoga kwa JK, msituletee kero tena za vurugu zake
 
1 JPM

2 LISU


3.MEMBE
Tusitegemee mchuano mkali kabisa kati ya jpm na mgombea mwingine yoyote kutoka vyama vya upinzani kwakuwa tayari sehemu kubwa ya utekelezaji wailani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi umetendeka, kadhalika na yale yaliomo katika ilani ya vyama vingine.
wanao Dhani lisu ataleta ushindani wanaudhaifu katika kumtazama lisu as presidential candidate, kwa sababu hoja nyingi za bwana lisu si zakuinua uchumi bali zakunusuru wapinzani na kiu ya raia si hiyo.

Kila la kheri Tanzania kila la kheri Mtanzania mlinda Amani
 
Siamini ka hao police wamefanya kwa kua wameelimika, ila ile barau iliyowafikia wameogopa wakifanya ujinga pesa zao walizohifadhi uko nje zitachukuliwa
 
Hapana Yule alikuwa Raisi wetu, Lazima twende kumuaga.

Hilo sina tatizo nalo, je bado kuna mahusiano mazuri baina ya pande mbili? Nina hakika Lissu akiingia hapo hilo zoezi litageuka na kubeba hali ya kisiasa zaidi. Ila kama ataenda, na ikatokea bahati mbaya akapewa nafasi ya kuongea, ni vyema akadhibiti ulimi na hisia zake. Ni ukweli usiopingika kuwa Lisu haivi chungu kimoja na Magufuli, huenda hafla hiyo ikaweka tofauti hizo hadharani kwa namna hasi. Ni vyema ukatolewa ushauri kuondoa hizo tofauti kuwa hadharani, ama kila mmoja kulinda ulimi wake.
 
Hii ni akili kubwa tuwe tayari kulipongeza jeshi la polisi pale ambapo linasimamia maslahi makubwa kwa manufaa ya Watanzania wote. Leo hii wengi tulikuwa tuna wasiwasi wa Lissu kukamatwa na vurumai kubwa kutokea (kumbukeni threads za wazushi mbali mbali hapa jamvini) lakini hayo yote mabaya yaliyotabiriwa hayakutokea.

Tetesi: - Vyombo vya Usalama vilivyojipanga kumpokea Tundu Lissu

Mungu ibariki Tanzania 🙏🏽

Asanteni sana @tanpol !!! Tunawapenda SANA!! SISI ni watu wema!!! Tanzania ni YETU SOTE. Tusiruhusu maslahi ya WATU wachache watuvurugie UPENDO wa ASILI wa TAIFA LETU-Halima Mdee
 
Ukisema uongo itakusaidia nini.

"Niwape pole wanachama wa @ccm_tanzania kwa kuondokewa na M/Kiti wao wa zamani, huu msiba ni wetu sote, siyo wa Rais @MagufuliJP pekee na kwa sababu ni msiba wetu sote, kesho Mungu akijalia basi tusindikizane tukampe Mkapa heshima yake " - @TunduALissu.
 
nakuunga mkono mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…