Halima Mdee amefanya vyema leo kulipongeza jeshi la polisi, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali sababu kuchukua maamuzi hasi dhidi ya cdm.
Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano hii rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anapambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi lake binafsi. Ni juu yetu wapinzani kutumia kukubalika kwa Lisu kwa njia chanya kuliko kuvutana