Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Sawa. Lakini CHADEMA ilikimbia bunge kwa sababu ya COVID-19. Wewe mwenyewe akili unakumbuka hilo? Kwa nini CHADEMA walau kisingewahamasisha wafuasi wake kuvaa masks? Huoni kwamba katika hili CHADEMA kinacheza ngoma ya CCM?
.
IMG-20191218-WA0001.jpg
 
Naona wewe hufuatiligi mwenendo wa kesi hiyo ya mh Lissu
Makosa yaleyale waliofanya mwanzo ndo yanajirudia kunakitu tunaita kutokuacha alama au ushahidi kwa lugha nyingine mfano Inshu ya J nassari kufukuzwa ubunge au la mbowe na ishu ya kuvunjika mguu usiku dodoma Sasa ndo hapa chadema wamefeli kuweka karata zao vizuri wanajua lisu anakesi mahakamani na wadhamini wake kila tarehe ya mahakamani wanaomba wajiondoe kumdhamini lisu sasa leo kaja ndo najiuliza hapa mahakamani haitatoa hati ya kumkamata lisu sababu anakesi mahakamani na wadhamini wake kila siku ya shauri uomba wajitoe kumdhamini?
 
PICHA KUTOKA JNIA

======

UPDATES;

1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.
View attachment 1518414
View attachment 1518413
Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati
View attachment 1518416
1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.
View attachment 1518415
1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu
View attachment 1518417
1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA
View attachment 1518418
1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.
View attachment 1518419View attachment 1518420
1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni
View attachment 1518423View attachment 1518422View attachment 1518421
View attachment 1518424
View attachment 1518425
1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.
View attachment 1518426
Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege itawasili

View attachment 1518431

View attachment 1518432
Hakyamungu Chuma kimetua, jamani MUNGU yupo, muuaji anajisikia vibaya sana saa hii, analia machozi na mda wowote mshtuko wa moyo unaweza mpata.

Acheni Mungu aitwe Mungu, loh, kuanzia leo naanza kusadiki Mungu yupo, anaishi!
 
Sawa. Lakini CHADEMA ilikimbia bunge kwa sababu ya COVID-19. Wewe mwenyewe akili unakumbuka hilo? Kwa nini CHADEMA walau kisingewahamasisha wafuasi wake kuvaa masks? Huoni kwamba katika hili CHADEMA kinacheza ngoma ya CCM?
Kwa wakati ule cdm walikua sahihi, kwa sasa umeona wangapi wanavaa hiyo kitu ?
Hii siyo Kenya

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
COVID-19 imeisha?! No more masks, no social distancing etc. Hapa ndio ninatatizwa na sera za vyama vya upinzani hapa nchini.

Inawezekana wanatumia Akili Upinzani,Moyo Serikali ya ccm.
Kwaio wanapinga kwa akili,wanafuata kwa utashi wa ccm.
 
Busara imetumika kuwaruhusu, natumai wanachadema wataheshimu sheria za nchi na kumsindikiza kipenzi chao sehemu husika baada ya kushuka.

Mama Tanzania ni mama yetu wote, tupendane.
 
Back
Top Bottom