Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Uzuri wa Uwanja wa taifa NI moja ya vitu vilivyo nifurahisha Sana. Kwa macho nimejionea mwenyewe. Pongezi kubwa kwa CCM na Marais Mkapa, Kikwete na hasa Magufuli.

Napongeza pia polisi kuwarusu wafuasi wa tundulisu wajionee wenyewe mazuri ya nchi.

Nachomuomba tundu Lissu lazima atembelee viatu vya Martine Ruther king. Katikati ya majaribu, thiki na anapoona hakuna haki ahubiri amani, Umoja na Upendo na kutoa hotuba za kuwashawishi watawala kutenda haki zaidi ya Alaiki ya watu kudai haki kwenye mazingira yasio Rafiki. Na inawezekana kabisa.

Naomba asijaribu kuwa Kama Patrick Lumumba wa Kongo. Akili ndogo ya kudai haki na nguvu nyingi ilipoteza kabisa Malengo yake binafsi na ya taifa lake.

Kuna kero nyingi za kusemea, nyingi mno adili nazo hizo. Asisahau kuhubiri msamaha kwa watu. Aseme wazi amawasehe wote waliotaka kumuua. Awasibitishie Viongozi wote wa Dola na Serikali watakuwa salama mno yeye akiwa madarakani. Aseme amemsamehe kila mtu kwa tukio lake. Na atusihi tusameheane. Akika atakuwa na hotuba zenye mvuto na kuponya wengi Sana.
Asisahau kuwasemea Wakulima wa:

•korosho pembejeo na soko lao na malipo
•Pamba, kuanza kukopwa na kutokulipwa
•Kahawa Bei ndogo kuliko uganda
•mahindi tuuze sembe na chakula Cha mifugo nje kiingeza garama.
•alizeti tuuze mafuta na Bei iwe nzuri.
•mitaji na mazingira Bora kwa boda, ma lishe, wachuuzi na wengine.

KIKUBWA FANYA TAFITI KWA KILA KUNDI SIO KUWASEMEA SHIDA WASIOKUWANAZO. KERO ZAO NI ZIPI. WAO WANATAKA NINI.
SEMA WANACHOTAKA KUKISIKIA SICHO UNACHOKIWAZA


Yale ya katiba mpya na tume huru Wajumbe kwa elimu yao hawataweza kukuelewa kaka labda uhusishe moja kwa moja na matatizo yao. Wajumbe usiwaletee ujuaji sana
 
Back
Top Bottom