Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Polisi wamewapuuza, mjichape bakora wenyewe sasa na mjipeleke central wenyewe. Hapewi kiki mtu yeyote hapa..mlitegemea polisi wanase ktk mtego wenu, imebumaaaaa....nna tumeamua lisu hashikwi ila wadhamini wake ndio watamgombania kama mpira wa kona..
Hamna lolote wewe, wamepuuza kitu gani?
Polisi siku zote ndo chanzo cha vurugu
 
Rudi kwa mada ya leo.. hakuna kukimbia.. nakuona una lia lia kwa viposti byako..[emoji2][emoji2][emoji2]
.
tapatalk_1577134048980.gif
 


Salaam Wakuu,

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara Tundu Lissu anatarajiwa kuwasili nchini leo saa saba na dakika ishirini saa za afrika Mashariki.

Lissu amekaa nje ya nchi miaka mitatu sasa baada ya kuondoka kwa shambulio la risasi lililotokea mjini Dodoma ,Septemba 7, mwaka 2017, saa 7 mchana, Area ‘D’, kwenye nyumba ya makazi ya viongozi wa Serikali mjini Dodoma.

“Lissu kwa sasa anatimiza mwaka wa tatu na anarejea hapa nchini baada ya kupona kikamilifu. Watanzania na wanachama wa Chadema wanakutana hapa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kwa lengo la kumpokea makamu mwenyekiti wa chama chao Lissu.

Hivyo timu nzima tupo hapa kukuletea kile kitakachojiri kwenye mapokezi haya.

Stay tuned.

======

UPDATE (NOTE: Picha zipo post ya 2):



1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.


Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati

1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.

1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu

1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA

1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.

1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni

1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.

Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege itawasili

1357hrs: Abiria wameanza kutoka nje. Lissu bado hajaonekana

1430Hrs: Msafara unatoka Uwanja wa ndege kuelekea Makao Makuu Kinondoni mtaa wa Ufipa
View attachment 1518508
1450hrs: Msafara Umefika Kipawa tunaelekea TAZARA. Watu ni wengi. Speed ni 10k/h
View attachment 1518515
Msafara Unaongozwa na Vijana CHADEMA. Hakuna Polisi hata mmoja. Watu wanashangilia na kulia kwa furaha. Magari yanapisha msafara bila tatizo. Hakuna fujo bodaboda wanaongoza Msafara
View attachment 1518545
1520hrs: Msafara umefika daraja laMfugale. Barabarani hakuna Polisi.

Watashitakiwa kwa kuandamana bila kibali, take my word
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
ila chadema nimewavulia kofia

yani mpo mnaserebuka kabisa pamoja na msiba mzito uliopo😁😆😆
Msiba wa kafara za Bashite wataenda kumuaga hakuna shida ngoja wamfikishe lisu nyumbani kwanza kisha watoe siri ya kifo cha mkapa
 
Back
Top Bottom