Halafu ukiwaaambia wanasema eti wewe mwanaume yanakuhusu nini ?? Yananihusu nini, hivi watu hawajui kwamba Fashion Industry inalipa sana ?? Yaani unakuta Celebrity kaka mtandaoni matusi, skendo na utimu timu tu.
Mkuu kama unakumbuka Iggy Azelea alivyokuwa juu sana mwaka 2013-2015 halafu ghafla akapotea. Alionywa sana na menejiment yake kwamba aache hizi drama na utoto utoto mitandaoni. Yeye kila tweet lazima ajibu, mara atukanane na Azalea Banks mara Britney Spears. Alikuja kuporomoka na anajaribu kurudi lakini nafasi yake kashika Cardi B, yeye apumzike tu kwao Australia.