simba kupitia kwa ahmed ally wamesema hawatosajili mchezaji wa ndani this time,hizo tetesi ni batili
 
simba kupitia kwa ahmed ally wamesema hawatosajili mchezaji wa ndani this time,hizo tetesi ni batili
Watasajili akina sawadogo toka nje ya nchi. Kwahiyo wanawaacha wachezaji si chini ya 10 then watawareplace na wachezaji wa nje. Sijui kwa nini ila Binafsi namuona Ahamed Ally kama kichwa hakipo sawa au Kanjibahi anamlamba Makofi pale Msimbazi.
 
Klabu ya Azam FC imedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao, ni baada ya kukubali kutoa kitita cha dola 300,000 (zaidi ya Sh 710.5Mil) kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Luis Miquissone raia wa Msumbiji.

Mshambuliaji huyo aliyetolewa kwa mkopo klabu ya Abha inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia akitokea Al Ahly ya Misri hivi karibuni alitajwa kurejea Simba SC kwa ajili ya msimu ujao lakini ikaonekana fedha anayotaka alipwe ni nyingi.

Azam FC wanataka kukamilisha dili hilo la Luis, ikiwa ni saa chache baada ya kumsajili Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutoka Young Africans.

Mmoja wa mabosi wa Azam FC, amesema kuwa asilimia hamsini mazungumzo yamekamilika kati ya kiungo huyo na uongozi wa timu hiyo.
 
Wanachokifanya Azam ni jambo zuri kwa maendeleo ya mpira nchini , Kadri Azam atakavyoleta ushindani katika ligi itafanya timu Simba na Yanga kufikiria mara mbili zaidi katika usajili..
 
Sasa wale wazee wa kusubilia pesa ya maandalizi ya super cup ili wafanye usajili itakuwaje? Wametoa macho kuomba iyo pesa itoke haraka iwaokoe wamebaki kupatanisha wachezaji kwa mali kauli but wenzao wanaweka mpunga wanapita nao kama kipanga ligi ikianza watakuwa wameambulia masalia kutoka ligi za Rwanda na burundi🤣🤣🤣
 
Hao masalia wanamfanya yule anaetembea kama kavaa kokoko akae roho juu kwenye ufungaji wa magoli ikiwezekana kabisa akakosa kiatu msimu wa pili mfululizo ambao ligi kuu anashindwa na wageni wanzake waliokuwa wanafikisha goal 20+?
 
Tajiri namba moja yupo Msimbazi
 
Hao masalia wanamfanya yule anaetembea kama kavaa kokoko akae roho juu kwenye ufungaji wa magoli ikiwezekana kabisa akakosa kiatu msimu wa pili mfululizo ambao ligi kuu anashindwa na wageni wanzake waliokuwa wanafikisha goal 20+?
Kupanga ni kuchagua wengine wana waza ubingwa wengine kiatu
 
Bila ya salamu

Habari kutoka vyanzo vyangu vya ndani katika klabu ya Wekundu wa Msimbazi zinaarifu kuwa Mshambuliaji hatari raia wa cameroon aliyekuwa akiitumikia klabu ya Rayon Sports nchini Rwanda, Willy Essomba Onana amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Wababe wa Tanzania, Simba Sports Club.

Usajili huu si tu utaiongezea makali ya ushambuliaji timu ya Simba Sc, bali utakwenda kupelekea Simba kuwa tishio katika kombe la klabu bingwa barani Africa. Muunganiko wa Onana na Jean Baleke utapelekea maafa kwenye timu pinzani na si ajabu tukawaona wawili hawa wakimaliza ligi wakiwa na magoli zaidi ya 50 kila mmoja.

Bienvenido Onana.

We are unstoppable
 
Hakuna mchezaji wa maana hapo.

Hana tofauti na Kyombo.

Muda utaongea

Wapenzi wa Simba tumechoshwa na maneno ya uongo kila msimu wa usajili unapofika, kiufupi msitegemee makubwa toka kwake labda itokee bahati tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…