Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA waendelea, Kawe kumewaka moto leo

Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA waendelea, Kawe kumewaka moto leo

Chadema tafuteni ushauri kwa dada Mange na Shangazi + Rwaitama + bagonza, munga na mwamakura kisha tounane wiki ijayo.
 
Nacheeeka huku naogopa!

Ndugu zangu wa CHADEMA jitoeni tu maana mpaka hapa mlipofikia mmeshafeli kwenye kambi zenu za upinzani mna watu hawa? Je, ni vipi mkifika maeneo ya Dodoma, Mwanza, Unguja na mengine ambapo ni kambi za CCM itakuwaje si ndo mtapata aibu ya mwaka?

Toeni hoja wananchi tujae kuwasikiliza ,matusi hayatawajenga kwa lolote lile na mtanyooshwa kisawasawa na wajumbe mwaka huu.

Anyway, ngoja niondoke hapa MKUTANO gani huu?

Kura yangu ni kwa yule anayejenga hoja tu
 
Mbona amtaki kuweka picha za leo hapo kawe?
Au ngoja niende nikapige mwenyewe,si ni viwanja vya Tanganyika packers tu hapo.
 
Ili kuweza kujenga hoja ni lazima ushabiki na misimamo ya ajabu tuiweke pembeni.

Bado sijajua ni kwanini awamu hii muitikio umekuwa ni hafifu mno aiseee.

Tukae chini na kujiuliza ni wapi shida ilipo.
Mnaposema ACHIENI MIKUTANO MUONE, wakati kipindi hicho badala ya kujenga sera mko bize kusubiri jpm kakosea wapi mdandie! Wananchi wa sasa sio wajinga, wana sense of organs zote na akili juu kutafakari...
 
hadi uzuni kweli kazi ipo
Na ipo hasa.
IMG_20200829_141307.jpg
 
Sasa hiyo mnakuwa mnawatenga wa nyuma hawaonekani mkuu, mmechukuwa tu wa mbele na anga kana kwamba wanaenda mbinguni, wekeni aerial view inayoonesha washiriki wote kabisa.. vivuli vinaonesha kabisa jua likielekea kuzama yaani ni kuelekea mwisho wa mkutano mkuu. View attachment 1551691
Wanatosha sana, tutapiga kura ndio la muhimu.
 
Nipo kwenye mkutano hapa na nimefika muda mrefu sana ili kusikikiza sera mbadala kutoka kwa viongozi wetu na mgombea wetu.

Kabla ya yote jana mgombea wetu alitueleza kuwa tutafanya maandamano ya amani kabla ya mkutano kuanza ila ukweli ni kuwa hatujafanya maandamano hadi sasa na tupo hapa hatujui kinachoendelea.

Mbaya zaidi hadi sasa mgombea wetu hajafika hapa kwenye mkutano na tunapata tu tetesi kuwa eti hajisikii vizuri
Watu tupo wachache kuliko jana mbagala, ila hii inaweza kuwa bahati mbaya kwa sababu nadhani wamechagua sehemu ambayo haikuwa sahihi.

Kawe ni sehemu ambayo imezungukwa na sehemu za ushuani ambao huwa hawapendi kabisa mikutano ya kisiasa. Ningekuwa mimi huu mkutano leo ungefanyika ubungo, magomeni au kimara lingetafutwa eneo zuri la wazi maeneo hayo kwa ajili ya mkutano.

Ila yote kwa yote kuna shida ndani ya chama.
Acha kushuhudia uongo wee kenge ...lini ukawa mwana Chadema? Uongo unakusaidia nn
 
Back
Top Bottom