Stan Mashamba
JF-Expert Member
- Apr 22, 2020
- 3,183
- 2,479
Wenye akili mgando ndiyo basi tena.Dada Victoire! Nimeona umekomalia hili la kuwaomba wanadi 'sera' zao sana. Bado kuna mapingamizi/ kuenguliwa kwingi hakujatolewa uamuzi na Tume. Ni zaidi ya hao wabunge 18 waliotangazwa jana na Tume kupita bila kupingwa. Wakianza tu kunadi sera kama unavyowahimiza na itokee Tume ibariki huko kuenguliwa kote kwa wapinzani ushindi wa uchaguzi unakuwa umeshaenda chama tawala kupitia meza za Wasimamizi wa uchaguzi na Tume. Unahitaji kujiondoa ufahamu ili kuendelea kunadi 'sera' katika mazingira ya aina hii. Kwenye hili wamefanya uamuzi wenye tija.......ingawaje itachukua muda kwa baadhi ya watu kuuelewa........