Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Ukienda TAKUKURU Upanga kuna watanzania wenye asili ya India kama watano walileta malalamiko pamoja na kadi za gari... Kuna mmoja alichukuliwa new model v8 ya mwaka 2016 na bei yake mpaka leo ipo juu sana hiyo gari..

Hawa walikuwa wanalindwa na mfumo ulivyokuwa wa nchi...

Kwani watu hawakusikia msemo huu ' KWENYE UONGOZI WANGU TAJIRI ANAFANYWA CHOCHOTE ' na watu wakapiga makofi..

Bora hawa wakina GSM wamesalimika na roho zao.... Matajiri wengi walifariki wa pressure kitokana na kuambiwa inahitajika hii.. Account yako inatakiwa ikatwe hela hii.....

Hujakaa sawa unafuatwa mheshimiwa amenituma kwako kuchukua hiki... Nk
Duh!!?
 
Mkuu wanasiasa si watu wa kuweka nao bifu hasa unapokuwa mfanya biashara. Kama GSM wana mtu wa PR wataliona hili nalosema. Hivi nani alijua Makala atakuja kuwa mkuu wa mkoa wa Dar???? Ninachomaanisha hapa ni kuwa wanasiasa wana mitaji mikubwa ya network, mtu anaweza kuwa idle kwa muda ila siku mtu wake akimkumbuka basi anaweza kulipiza kisasi. Msipe kichwa GSM. Na kumbukeni Makonda na Mama ni kitu kimoja.

Nimeelewa mkuu
 
Record yao chafu haiwazuii kuchukua nyumba yao iliyotaka kutapeliwa na bashite.
Mbona hawakusema toka mwanzo kua Makonda anawalazimisha wamjeengee hiyo Nyumba! Hao wote wanajuwana kwenye ma deal yao machafu! Na si muda Siri zao wote watazitoa kwa jamii, ili mjuwe aina ya Viongozi na Wafanyabiashara mnao waamini sana!!
 
Kama mtu ni division ZERO hakika hawezi kuficha ZERO yake maishani. Makonda amekuwa mfanyakazi wa Serikali kwa miaka 2014-2020, ni kwa mshahara gani anaweza kumiliki nyumba ya Tsh 2.0 Billion?

Angekuwa ana akili hata ya Div IV, ingebidi akae mbali na utajiri huu na azoee maisha ya kawaida.

Hata kama Rais SSH anamlinda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, ajue tu iko siku Samia atatoka madarakani na ATADHALILISHWA tu. Mali ya DHULUMA na damu za watu wasio na hatia alizomwaga bado zinamtafuta
Mbona kuna Watumishi wengi tu wa Umma wanamiliki Mali ambazo haziendani na vipato vyao!? Au wwe Tanzania umekuja juzi!? Hii point yako futa kabisa,labda uje na hoja nyingine!!
 
Raha zinaisha taratibu mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Watu huwa wanajidanganya tu ! Duniani hakuna raha inayonunuliwa kwa gharama kubwa !! Raha ya dunia ni kupata peace of mind !! Na hiyo peace of mind huwa hainunuliwi kwa bei yeyote !! Maneno yangu haya wenye utajiri wao wanajua kuwa nasema kweli !! Ila wale ambao hawajawahi kupata utajiri hawataamini maneno yangu haya !!
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Kama Makonda alifikia kutumia jina la JPM kujimilikisha visivyo halali na kudhulumu vya wengine hatakiwi kuonewa huruma.

Na hii inachafua uongozi uliopita. Kumbe watu walikuwa wanajiamulia.! Maadamu vyombo vya usalama vipo basi ukweli utajulikana.

Kweli tutasikia na kuona mengi
Mbona Makonda hakukufuata wwe umjengee Nyumba kipindi cha Magufuli!? Kwa kuwa wwe hutaki Ulinzi wake kwenye biashara zako,labda kwa kuwa huna biashara chafu! Wafanyabiashara Wenye biashara chafu ndiyo hutegemea Viongozi wawalinde ili ma deal yao yaende! Huyo GSM na Makond kila Mtu afunguke au wenyewe warudi tena kwenye meza ya makubaliano bado hawajachelewa!!
 
Back
Top Bottom