Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Unajua kuna makosa ya kibinadamu kiasi kwamba hata ukikosea unaweza usijutie sana.

Ila broo kwenye kubeti siyo kosa la kibinadamu ni tamaa na kujiendekeza tu.

Inaniuma sana kupoteza pesa kwenye kubeti.

Ni bora hata ningekamatwa huko na dawa za kulevya nikafungwa nisingeumia sana maana nilikuwa natafta utajiri japo kwa njia haramu.

Ila kubeti milion 7.5 kwa siku 5, kuna najidharau sana natamani hata nijichome visu vingi tumboni maana najiona sina akili hata ile moja
 
Hakuna kosa lisilokuwa la kibinadamu chini ya jua, unaweza ukamuamini mtu na akakufix ukaishia kupoteza kila kitu kama ilivyokuwa kwangu. Cha msingi ni kukubaliana na kilichotokea na kusonga mbele. Hilo ni funzo kubwa sana kwa maisha yako, lifanye kuwa ngazi ya kupanda juu zaidi.
Kuna mzee wangu mmoja, alikuwa ni tajiri mkubwa sana miaka ya 80, operesheni uhujumu uchumi ikamfilisi kila kitu hadi akawa anatembelea baiskeli. Alikuwa akichekwa na kudhihakiwa, kutoka kumiliki gari za mizigo (Scania) miaka hiyo, na biashara zingine kibao. Kuna wenzie walijitoa roho yule mzee alikomaa, ikatokea bahati ya biashara ya Sangara miaka ya 90 mwishoni kuelekea 2000, akatoboa ile mbaya.
 
Aisee
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 qmmmmk jamaa unawaza ngono tu
 
Virtual bet ya betpawa ni fake na haina uhalisia kwani kitu kimoja kinamatokeo tofauti i.e game moja inamatokeo tofauti. Virtual ni uwongo nimetafiti vya kutosha sana.
 
Ninachoshukuru sijui kuendesha kindege, sijui kuzungusha lile tairi na wala sijui kucheza dubwi la mchina.

Ila kuna siku nimewahi kupoteza laki 2 kizembe sana ilikuwa 2020 kama sikosei.

Ni kupitia 1xbet nilikuwa nimebet football nikala.
Sasa ukatokea ujumbe kuwa naweza kudouble my winning, nikakubali.
Ukaja mchezo wa kupiga penalt halafu kuna goalkeeper anadaka.

Ninachokumbuka nilikula kama mara 2 tu, nyingine goalkeeper alikuwa anadaka na kutema hadi nikakauka kau.
 
Virtual bet ya betpawa ni fake na haina uhalisia kwani kitu kimoja kinamatokeo tofauti i.e game moja inamatokeo tofauti. Virtual ni uwongo nimetafiti vya kutosha sana.
Upo sahihi ni virtual games ni computer inasetiwa imnyooshe mtu,ukitaka kujua kaeni wawili wekeni matokeo mawili tofauti mechi iyo iyo muone kama mtashinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…