Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Hivi kuna nini CCM wameambiwa wasiwe na tamaa ya uongozi, lakini wameshindwa uvumilivu wa mchakato wa kisiasa wa kuteua wagombea ngazi ya kwenda kugombea udiwani hadi wanashikana mashati
Aliyewaambia wasiwe na tamaa ya uongozi yeye ni wa chama kipi? Na je yeye hana tamaa ya uongozi?

Viswali viwili naamini utavijibu.
 
Wanaoandamana ni chadema siyo CCM
Laana itawatafuna maishani mwao wote wanao fanya ubaguzi kwenye nchi yetu mzuri tulio achiwa na baba wa taifa mwl JK Nyerere ikiwa na upendo na amani na mshikamano
 
Upinzani wajiandae kuwapokea wageni, mamia kwa maelfu.
UJANJA AMBAO CCM WAMEUFANYA MWAKA HUU, WANATAKA WATANGAZE MAJINA TAREHE ZA MWISHO WA KUCHUKUA FORM ILI UKIKATWA HATA UKIKIMBILIA UPINZANI UNAKUTA FORM HAZITOLEWI TENA SABABU MWISHO WA KUCHUKUA FORM NI TAREHE 25/08/2020.
 
18 Aug 2020
Dodoma, Tanzania

WanaCCM waandamana kupinga maamuzi



Vurugu zinaendelea leo 18 agosti 2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kupokea majina ya wagombea udiwani ambao wamekatwa licha ya kuongoza.

Jana halmashauri ya CCM mkoa wa Dodoma walirudisha majina ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho ambapo kata 7 Kati ya 41 za jiji la Dodoma walioongoza walikatwa na kurudishwa wengine ndipo wakaandamana ofisi za wilaya.

Mmoja wa diwani aliyeshinda CCM lakini jina lake lililokatwa amewaomba wanaCCM wa kata ya Changombe kuwa watulivu wasifanye maandamano wasubiri maamuzi ya Halmshauri ya wilaya CCM watakapotafuta ufumbuzi wa sintofahamu hiyo ndani ya CCM .

Chanzo: Mwananchi digital

Nimechekaaa Eti "...acha useng..." 🤣
 
Serikali na chama idhibiti hawa wahuni, kuna mwaka huko nyuma tulishauziwa mbuzi kwenye gunia eti kwa watu kuhofiwa kuleta vurugu. Waende mbali kuchunguza hao wafanya vurugu wasije kuwa wamelipwa. Mtu anaye honga wajumbe atashindwa kuhonga waandamanaji ña wafanya vurugu. Tusipokuwa makini kama Taifa tutapata viongozi wahuni Safi sana Polisi msicheke na nyani kwenye shamba la mahindi. Wako watu walishafanya taifa hili shamba la bibi.
 
Laana itawatafuna maishani mwao wote wanao fanya ubaguzi kwenye nchi yetu mzuri tulio achiwa na baba wa taifa mwl JK Nyerere ikiwa na upendo na amani na mshikamano
Mungu atusaidie hali si nzuri ila malipo ni hapa hapa duniani
 
Back
Top Bottom