Wadada siku hizi wanatongoza, hawana aibu tena

Wadada siku hizi wanatongoza, hawana aibu tena

Hii ndo nzuri sasa ! Kusubiria mtu amfuate inachosha sana , sasa akae benchi mwaka wakati anaona kabisa kuna muhuni pembeni kamuelewa !! Na wanaomfata hawaelewi ! Na wahuni wengine ni wazito analetewa hadi gheto anajifanya haoni 😂😂 Na wanaume tuondoe hofu sio kila demu anayekutaka ana tabia mbaya !😂 Nyonyoa kuku huyo ,kienyeji ni tamu sana.
Wasalaam
Mbaya zaidi, yeye anaweza akakuelewa ila wewe hujamwelewa (kuvutia).
 
Kuna siku nilitembelea chuo fulani, kwa ajili ya shughuli tu za kikazi.

Ile nikiwa kwenye foleni katika kusubiri huduma, nikakutana na jamaa zangu wawili ambao tulikuwa tunafahamiana huko mtaani; tukawa tunaongea na kubadilishana mawazo ya hapa na pale.

Mara akaja mkufunzi mmoja wa kike, akatupa hai, tukawa tunaongea huku tunacheka. Mara yule mkufunzi akaniuliza, ''huna mdogo wako aje anioe, nimechoka kuwa mwenyewe''. Nilishtuka ghafla kutokana na huo ujasiri aliokuwa nao, mpaka kunitamkia hayo maneno bila kupepesa macho.

Nikamuuliza, uko siriazi? Akanijibu, ndio; nami nikamjibu, ''kwa bahati mbaya wote walishaoa, na wakike walishaolewa''.

Ila katika kutafakari, nikahisi ujumbe ulikuwa unanilenga mimi, kwa sababu huwa nikitembea huwa sivai pete ya ndoa.

Ikabidi nimjibu kwa kifupi, nitakutafutia.

Swali langu; kwa nini nyakati hizi wadada wamekuwa wepesi kuwafungukia wanaume?
Thread kama hizi zinafanya wadada wapunguze kufunguka...
Tanzania ndo bado tunashangaa..
Wadada Kenya na kwingineko kutongoza akikuelewa kawaida sana
 
Back
Top Bottom