Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Kisa changu kinaanza baada ya kumaliza form six shule x jijin Mbeya nikaenda kwa brother huko Dar. Ebwana enhee! Kufika huko nakuta life imebamba kinoma yaani tunalala room moja na kila asubuhi kumi na mbili natakiwa kufuata maji na kuwasambazia wateja majumbani mwao kwa kila dumu kipindi hicho linauzwa 150,ilikuwa shughuli pevu haswa.

Sasa nikabuni utaratibu wangu kuwa mteja maji atafuata geto na si kupeleka kwake,weee broo alikuwa mbogo balaa. Huku nikitafakari nini cha kufanya broo naye aliniahidi kunitafutia kazi,mie nikawa na mzuka wa kazi balaa. Mara naambiwa andika barua kwa anuani hii,haaa nashangaa ni anuani ya makampuni ya ulinzi,nikajisemea moyoni hivi kweli mimi nakarisk maisha kirahisi hata mafunzo ya kushika kirungu sina. Broo akaniongoza kwenda kunionesha ofisi za kamapuni hiyo na kutakiwa kesho yake nikafanye usaili.
Sasa siku iliyofata nilikamata gari huyoo kwenda zangu beach kupunga upepo hata sikusogea lilipo lango lao najioni nikarudi nikiwa na majonzi kibao kuwa wamenikataa kisa mi mfupi kumbe fix tu.

Mbilinge nyingine nikawa nahangaika na matangazo ya kazi magazetini,ghafla vuuup nakuta tangazo la kazi ya marketing katika kazeti sijui ilikuwa nipashe sijui,kidume fastet nikaandika kabarua kangu na kizungu changu cha ugoko huyo mguu kwa mguu mpaka zilipo ofisi zao nadhani mitaa ya tazara kule. Kufika tukapigwa usaili wa kizushi ndani ya dk 5 tunaambiwa kazi mmepata na mnatakiwa mkabiziwe kwa wazoefu wawafundishe kazi kwa vitendo.

Kimoyo moyo najua nimelamba dume kumbe chenga kabisaa,nikakabidhiwa kwa mdada flani na mabeg mawili ndani yamejaa mafuta,dawa za meno ,miswaki n.k tukaanza safari huyo mpaka mitaa ya kigogo huko tukadrop na kuanza kupita majumbani kwa watu na kunadi bidhaa,nikasema mmmmmhh hii ngumu kumeza. Tulizunguka kuanzia saa mbili mpaka saa saba hakuna kitu kilichouzika nikasema mama yangu huku nako choo cha kike na nimeshachuchumaa tayari. Nikawaza hapa nimpige fix takatifu nimtoroke tu huyu dada,kweli nikamdanganya nimeondoka na funguo ya geto wakirudi hawatanielewa kabisa. Kwa shingo upande akaniruhusu niondoke akanipa 200 ya nauli huyooo mpaka geto na jwa hasira nafika nilikunywa maji lita moja na nusu.

Nashukuru Mungu matokeo ya six yanatoka nikawa nimechana fresh nikamshukuru sana Mungu kwa kuniepusha na kikombe kile kwa wakati ule. Mungu ni mwema ile namaliza chuo tu sikuwahi kwenda home nikapitiliza kazini katika shirika y na kuanza kupiga kazi na kamshahara hakukuwa haba na nyumba nikapewa juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Hasira ukanywa maji Lita moja na nusu[emoji16][emoji16][emoji16]

Typed Using KIDOLE
 
Aisee hongera sana mkuu,umenifurahisha sana ulivyoandika.
 
Tola uzi wa masiahala umeleta mawazo chanya kubuni thread zenye mantiki pia eeeh.... Dzain zinaendana kimtindo jinsi ya kuuliza kitu.

MashineNene[emoji533][emoji1646]
 
Tola uzi wa masiahala umeleta mawazo chanya kubuni thread zenye mantiki pia eeeh.... Dzain zinaendana kimtindo jinsi ya kuuliza kitu.

MashineNene[emoji533][emoji1646]
Hahaha ule uzi ni balaa mkuu
 
niliajiriwa na shombe fulani kutembeza mayai ya kuchemsha, niliuza siku moja, hesabu sikumpa na mayai yaliyobakia tukayala yote na ndugu zangu.
 
Umetaja mitaa yangu hiyo mkuu,alienilea alikua humo ndani TRA kwa miaka kama 7 hivi namimi pia niliwahi piga fild apo pia mwaka 2016
Pamodz nilipata kadada fulani kasweet kalikuwa nkanaitwa Salma. Kalikuwa na wivu hako, balaa.

Ughonile malafyale
 
Mzee wa bh. Bila shaka ulikua mapinduzi dom. Nilikua PCB 2 ya kwanza kabisa ya kadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POLE SANA----------------------------------inaelekea ulikuwa hulijui hili.;

Nikikumbuka kipato changu chote miaka 9 nimeishia kuwasomesha wadogo zangu ambao kwa Sasa wananidharau inanouma
 
Meuza kuni mimi jamani, mbaya zaidi wanunuzi wanajiongezea kuni, wanalalamika ila namshukuru Mungu kwa kweli nilifanikiwa kuvuka salama kwenye mapito!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanunuzi wanajiongezea kuni
 
Sio kuuza tuu, nilienda kuzifuata msituni ndo nakuja kuuza!!

Kabla ya hapo nilikuwa nahubiri sokoni, kwenye vituo vya mabasi sadaka ikawa hainitoshi nikaamua kwenda msituni kukata kuni na kuuza!
Shikamoo dada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…