Wanaoondoka CHADEMA ni waliokuwa Viongozi peke yao, Vipi Wanachama?

Watu wanachekesha,kama alishindwa 2015 anategema kushinda uchaguzi upi huo?
 
Hivi dunia imeamua kisa tundu lissu
 
Una hakika kuwa wote wanaohudhuria mikutano ya hadhara ya CDM ni wanachama wa CDM?

Amandla...
Ndio uelewe kuwa No Reforms No Election ni kwa maslahi ya Tanzania bila kujali chama wala dini, na ndio maana wanaohudhuria mikutano ya NRNE ni Watanzania.

Suala la watu wengi kujitokeza kwenye mikutano ya NRNE bila shuruti, bila kuzolewa na malori na bila kuwepo wasanii, ni kielelezo kuwa CHADEMA inakubalika.
 
Ndugu yangu Mohamed Said, habari za siku nyingi. Nadhani tunajuana vizuri tu...tumetoka mbali na tumewahi kuwa na minakasha si haba.

Nyakati nyingi hatukukubaliana lakini kwenye jambo la wazi kama hoja uliyoiweka hapa tuko pamoja lakini kwa tofauti dogo tu katika mtazamo,

Mtazamo huo unaoutofautisha ni mdogo sana lakini una ujumbe mzito; wakati wewe unashangazwaa kwa yanayojiri, mimi sishangai hata kidogo.

Sishangai kwa sababu niliyategemea haya na sasa yanatokea kama nilivyoyatabiri. Mimi siyo nabii ila huwa najifanyia tafiti zangu japo si mtafiti kwa maana ya kusomea.

Katika lugha ya Kiingereza kuna maneno mawili yanayoelezea ukweli, fact na truth. Neno ukweli (fact) linahitaji ushahidi (evidence), lakini neno ukweli (truth) huwa ni self-evident.

Katika utafiti wangu uchwara, nilimshauri Mh. Mbowe asigombee kulinda heshima yake aliyoijenga kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka ishirini!

Hata Mh. Mbowe mwenyewe awali, toka 2019, alionesha kusita kugombea lakini vongozi ambao kwa sasa ndilo hili kundi linalojiita G-55 walimshauri tofauti.

Kwa mara ya kwanza Mh. Mbowe akaonesha udhaifu ambao ulituacha wengine tulio na nia nzuri midomo wazi. Na sasa Mh. Mbowe anavuna alichopanda.

Chadema ilichagua uongozi mpya katika uchaguzi ulioendeshwa kwa haki, uwazi na bila mizengwe aina ya tuliyoishi nayo kwa kipindi kirefu toka mwaka 1995.

Niliposikia dukuduku za waliojiita G-55, niliwapa tahadhari wasi-underestimate nguvu na ushawishi waliokuwa nao viongozi wapya kwa wananchama wa Chadema.

Hii ni Chadema mpya, chama cha wananchi ambacho kila mwanachama kwa uchungu wake yuko tayari kupitia TONE TONE kukichangia hata kile kidogo alicho nacho.

Namshauri tena Mh. Mbowe asione haya, hajachelewa, aachane na kakikundi haka ambacho kiko tayari Chadema ife lakini mikono yao iende kinywani, aluta contonua!

Chadema haisambaratiki labda nguvu ya ziada itumike kuwateka, kuwaua na kuwapoteza mamilioni ya wananchi ambao kwa sasa ndio wafadhili wakuu wa Chadema.
 
Yaani unatabiria mabaya tuu kuhusu CHADEMA huko mbeleni!!
Itakuwa hivi, itatokea vile!!??

Nastaajabu kwa ndugu yangu FAM mwenye akili nyingi kuzungukwa na watu wengi wenye akili fupi na roho mbaya tofauti kabisa na yeye.
 
Sio mara ya kwanza watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya vyama vya upinzani. Swali ni kuwa wako tayari kujitolea kiasi gani kutetea chama chao na wao?

Amandla...
 
Reactions: Tui
Yaani unatabiria mabaya tuu kuhusu CHADEMA huko mbeleni!!
Itakuwa hivi, itatokea vile!!??

Nastaajabu kwa ndugu yangu FAM mwenye akili nyingi kuzungukwa na watu wengi wenye akili fupi na roho mbaya tofauti kabisa na yeye.
Mimi nasema ninacho kiona. Siko hapa kumfurahisha mtu. Mwenendo wa Chadema ya leo hainipi matumaini. Chama chochote kinachoendekeza visasi, kejeli na kuto kukubali kukoselewa kinakuwa na mwisho mbaya. Mpaka sasa hivi mbali na matusi,

Chadema imeshindwa kujibu hoja za G-55. Kwa kifupi, watahakikisha vipi kunakuwa na No Elections maana wote tunajua CCM haina mpango wa reforms zozote za maana kabla ya uchaguzi. Wangepewa jibu linaloeleweka wasingeondoka.

Amandla...
 
Reactions: Tui
Yaani unatabiria mabaya tuu kuhusu CHADEMA huko mbeleni!!
Itakuwa hivi, itatokea vile!!??

Nastaajabu kwa ndugu yangu FAM mwenye akili nyingi kuzungukwa na watu wengi wenye akili fupi na roho mbaya tofauti kabisa na yeye.
Huyu John Mrema anakuwaga mjinga fulani.
 
Huwez kulitatua tatizo kwa kujifanya halipo, busara ni kujua chadema ikipoteza ni sisi tunapotea. Ni ujinga kuamin kuwa huhitaji mtu kufikia malengo yako. Dunian tunahitajiana mzee. Hakuna kaz ngumu kama kumtengeneza kiongozi hasa wa upinzani. Kutengeneza wafuas ni jambo dogo. Ila mfuas kujitoa sadaka kwaajili ya nchi sio jambo rahic. Kwa mfano chadema itabid wakimaliza mikutano warud kwenda kufanya uchaguz kila mahali uongoz ulipotoka then ndio waje kujipanga na no reform no elections. So by the time hakuna mtu wa kuwaunganisha watu kwaajili ya kuzuia huo uchaguz. Huhitaj akili kubwa kujua chadema imestak. Kwa mfano watu wana hasira na ccm. Na wanakuja kwenye mikutano coz wanawasikia watu wakiwaponda ccm. Sasa swali linakuja hiv, what if ccm ikaiwezesha chauma kwa mfano wakapata baadhi ya wabunge na wa viti maalum, then wakawasemea wananchi kama hawa hawa wa chadema je unataka kuniambia wananchi bado watakuwa nao? Hiv watu wanasahau watz ni mabingwa wa kusahau? Au wamesahau hata wakat wa uhuru hakukuwa na TANU peke yake kwenye mapambano ya kupata uhuru? Ni ujinga tena sana kutumia mbinu zile zile ukitarajia majibu tofauti.
 
Wanaoondoka ni wachumia tumbo lakini wapambanaji wanazidi kuongezeka. Tena kwenye mikutano inayoendelea siyo watu ni wengi tu lakini wanatoa michango yao kusaidia operesheni No Reforms No Election.
Halafu wote ni kutoka kanda ya kaskazini tu. Kina minja, mrema nk. Kulikoni???
 
Uko sahihi Mkuu lakini sidhani kama G55 wataenda Chaumma. Huo mtego waliowategea wenzao na wakaingia kichwa kichwa.

Mimi naamini kuwa watajiunga na ACT-WAZALENDO. Hii ni kwa sababu ACT-WAZALENDO tayari wana infastructure nzuri kuingia kwenye uchaguzi. Weakness ya ACT-WAZALENDO siku zote ilikuwa upande wa bara hivyo G-55 wakijiunga nao watajiongezea nguvu.

Kingine ni kuwa Zitto hana ugomvi na Mbowe ambae bado anamheshimu kama mentor wake. ACT-WAZALENDO mpya itakuwa chama cha kwanza kitakachoweza kutoa upinzani mkubwq kwa CCM bara na visiwani.

Naamini Halima na Esther Bulaya watajiunga na ACT-WAZALENDO na watagombea kwenye majimbo yao ya awali. Aidha, kura watakazopata zitawawezesha kuwa na wabunge wa viti maalum wengi.

Baadae, Mbowe atatangaza kuwa Chadema sio mama yake na atajitoa na kujiunga na ACT-WAZALENDO. Ataondoka na wanachama na viongozi wengi. ACT-WAZALENDO wakimfanya awe mgombea wao wa urais, watavuna pia kura nyingi ambazo zitawaongezea ruzuku wanayopata pamoja na wabunge. Mbowe kugombea urais ambao anajua hatashinda ni strategy nzuri kwao.

Haya ni mawazo yangu na kuna uwezekano kuwa nimekosea kabisa.
CCM watakuwa wameshinda battle hii lakini washindwa war maana kwa sababu wameunganisha upinzani.

CDM watakuwa watazamaji tu na kuendeleza matusi dhidi ya Mbowe, G55 na ACT-WAZALENDO.

Amandla...
 
Kutakuwa na wimbi la wanachama na viongozi wa CHADEMA litakalo ungana na G-55. CDM itabaki hai lakini itakuwa inaelekea ICU.

Amandla...
Wanachama na wafuasi ni wachache watahama, viongozi litakuwa si jambo geni maana hata wakati wa kuunga juhudi walihama viongozi wengi, na vyeo wakapewa huko walikoenda, lakini ushawishi wa cdm umebaki vilevile. Labda hiyo agosti matamanio yako yatafikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…