Sorry to say this.
Mimi ni Mkristo, na nina kipato kikubwa kuliko mwenzangu. Lakini ninaishi maisha ambayo ni ya kimwambia Roho Mtakatifu, nipe unyenyekevu, nipe utii, nishishe, ondoa ndani mwangu kiburi, ondoa kujikukweza, mume wangu ni kichwa cha familia, hela si kitu kwangu, nipe heshima Mungu wangunifanyike mke mwema, kwa kweli huwa najishusha sana.
Kuna kipindi kiburi cha pesa kikaanza kujiinua, nikafunga na kuomba haikusaidia, nikapata jibu kwamba ni lazima account zote awe anaziongoza yeye.
Pia nikatoa nusu ya hela yangu yote nikampa afanye mtaji wa biashara zake mwenyewe.
Ni mwanaume mzuri sana ananifundisha na kunielekeza mengi amefanyika baraka sana maishani mwangu