Wanawake wa hivi bado wapo vijana oeni, ndoa bila shela yafungwa kanisani na kushangaza waumini wengii

Wanawake wa hivi bado wapo vijana oeni, ndoa bila shela yafungwa kanisani na kushangaza waumini wengii

Ukiangalia hii picha hii ndoa unaiona kabisa ina uhakika wa kudumu muda mrefu
 
Wanaume hawana shida inapokuja swala la kuoa. Shida huja kwa bibi harusi mtarajiwa, mama wa bibi harusi au/na mama wa bwana harusi mtarajiwa. Hicho kikundi tajwa hapo juu, hupenda makuu.

Si ajabu hao wakawa yatima. Au binti umri umeenda na bwana harusi hana maisha.
Au bibi harusi ana ujauzito na wanakwepa asizalie nyumbani
 
Mtu anajua kabisa hana kampan na hana uwezo wa sherehe,anaanza kulazimisha na kupiga sim kila saa kuomba michango.Ndoa sio sherehe ndoa ni watu wawili waliopendana,mkishapendana nendeni kwa viongozi wenu mfunge ndoa.Hizi kero za michango ni mbaya sana.
 
KIjana ameshinda pressure kubwa kutoka upande wa mwanamke akiwemo mwanamke mwenyewe na pressure ya wazazi hasa mama kutoka upanda wake. Hongera kwake​
Wanawake Wengine utasikia wanasema,"marafiki zangu watanionaje,mimi siwez funga ndoa hvyo bora tuache tu,nitawaibisha ndugu zangu"

Nimependa zaidi yaan bado ni vijana kabisa na wamefanya jambo la maana sana

Sio kama ndugu zetu wanaotumia mpaka 10mil huu ujinga,eti mpaka unawakodia ndugu gari la kuwarudisha baada ya harusi
 
Ndoa huwa hufanywa kulingana na maamuzi ya wanandoa.unaweza kuiamua kuifanya iwe ya gharama au isiwe ya gharama
 
Nimemuona Pastor Maotola Lumbe kwa pembeni hapo bila shaka hapo ni Kanisa la Kinyerezi SDA
Nawapongeza hao vijana kwa hatua hiyo kuliko kuishi sogea tukae bora walivyoamua kufunga ndoa na kupata baraka za mbinguni
 
Hao maharusi kama si wahaya watakuwa wachaga.
 
Itakuwa ni waliojikatia tamaa,walioko kwenye kilele cha ubora hata za bomani hawataki kuzisikia.
 
Back
Top Bottom