Wasukuma punguzeni huu ulaji wa chakula kingi namna hii

Wasukuma punguzeni huu ulaji wa chakula kingi namna hii

Huku wanawache wanavutambi ila usukukumani hakuna mwanamke mwenye kitambi.
usukumani mwanamke ni kama mnyamakazi, kunenepa sio rahisi,
uchagani mwanamke asipokula chakula anakula mabusu!
 
Mtu unakula msosi mnzito maana baadae unakwenda shambani kulima .Au Ndemi kila siku tunampikia ugali asubuhi na mariboto na Nkalango wenye nhwili za kutosha.Bugali Bo Ndemi .Hapo Ndemi anashinda machungani kirahisi kabisa.
 
Habari za Jumapili wakubwa.

Juzi kati nikamtembelea jamaa yangu fulani hivi ni msukuma anaishi nje kidogo ya mji.

Ebana sijawahi kuona watu wanakula kama hawa watu.

Imeletwa nguna ya watu watatu tu mezani lkn hiyo nguna kwa wanaume wazembe kama wa Dar wangeweza kula mwezi mzima.

Tumepiga nguna weeeee me nikasarenda nikawaacha wenyeji wakaisukuma mpaka ikaisha nikabaki mdomo wazi tu.

Ndugu zangu punguzeni huu ulaji wa ovyo namna hii.
Hao uliokutana nao ni wazembe. Baada ya hapo kulitakiwa kuletwe wali au viazi kama dessert. Itakuwa umekutana na wasukuma wa mjini mkuu😂
 
Sio Wasukuma pekee ndiyo Walaji wa chakula kingi. Nafikiri ni mikoa yote ya Kanda ya Ziwa ni Walaji wazuri wa chakula kingi.

Ulaji wa chakula kingi unategemea na shughuli mtu azifanyazo, kama utakuwa unafanya kazi nyingi za nguvu huna budi kula chakula kingi ili kupata energy ya kutosha kwenye shughuli zako.

Mimi pia nilikuwa Mlaji sana wa chakula nikiwa kule, baada ya kuja DSM nikapunguza kabisa.

Juzi nilipoenda Musoma kusalimia, nikakutana na msosi wa kula watu sita wa DSM lakini tukatakiwa kula watu watatu.

Kwanza walipakua wali Samaki tukala.

Baada ya dakika 15 wakaleta mezani ugali Samaki, eti walisema ule wali ilikuwa ni wa kuonja tu 🙌

Kwa kweli tunaoishi mijini ni kama hatuli kabisa, haiwezekani ule Chipsi sahani Moja eti ushibe, hizo nguvu za kuzalisha watoto 12 kama Wazee wetu zinatoka wapi 🙌
Hii pia nilikutana nayo sehemu, yaani sisi kama wageni tukatengewa sahani za vifusi vya wali na nyama za kutosha. Baada ya dk chache ikaletwa nguna na mboga kama zote. Wazee wanasema ile ya kwanza ilikuwa ni kionjo(yaani kuliandaa tumbo) kabla ya kupata chakula.
 
Mtu unakula msosi mnzito maana baadae unakwenda shambani kulima .Au Ndemi kila siku tunampikia ugali asubuhi na mariboto na Nkalango wenye nhwili za kutosha.Bugali Bo Ndemi .Hapo Ndemi anashinda machungani kirahisi kabisa.
Dah umenikumbusha bhugali bho ndimi, ugali wa moto, nkalango au nyama iliyokaushwa ( ng'homele) na mtindi ( malibhoto).

Tatizo la Nguvu za kiume utalisikia Daslama tu 😂😂😂😂😂
 
Wanaona sifa kula chakula kingi, wanasema kwao hakuna njaa wanalima sana. Mtoto mdogo anaanza kulishwa chakula kingi ili tumbo lipanuke awe anapakia chakula kingi hatimaye akiwa mkubwa awe na umbo kubwa. Mshangao ni pale wakienda chooni mtu anashusha kimba la kilo mbili! Kwa ulaji huo choo kitaachaje kujaa haraka?
😂😂😂😂
 
Hii pia nilikutana nayo sehemu, yaani sisi kama wageni tukatengewa sahani za vifusi vya wali na nyama za kutosha. Baada ya dk chache ikaletwa nguna na mboga kama zote. Wazee wanasema ile ya kwanza ilikuwa ni kionjo(yaani kuliandaa tumbo) kabla ya kupata chakula.
Hahaha..............kama umezoea misosi yetu ya town, ukishakula wali hutakuwa na uwezo wa kula tena hiyo nguna 😅🙌
 
Habari za Jumapili wakubwa.

Juzi kati nikamtembelea jamaa yangu fulani hivi ni msukuma anaishi nje kidogo ya mji.

Ebana sijawahi kuona watu wanakula kama hawa watu.

Imeletwa nguna ya watu watatu tu mezani lkn hiyo nguna kwa wanaume wazembe kama wa Dar wangeweza kula mwezi mzima.

Tumepiga nguna weeeee me nikasarenda nikawaacha wenyeji wakaisukuma mpaka ikaisha nikabaki mdomo wazi tu.

Ndugu zangu punguzeni huu ulaji wa ovyo namna hii.
Naipenda kabila yangu kinoma noma Wasukuma Juu, acha tule kabisa maana hata kulima tunalima sana .
 
We mshenzi sana, unaenda kwenye familia ya mtu unapikiwa unakula na kushiba kumbe unawachora watu wema na maisha Yao?

Unawezaje kuleta Uzi kumzungumziq mtu ambaye hakukutendea ubaya Tena anakula vyake?

Angekuja kwako Akala si ungefungua maelfu ya nyuzi?
Makabila mengine sijui mkoje, ufahamu wenu mdogo juu utofauti wa desturi za maisha.

Wasukuma ni wakulima wa mazao mengi ya chakula, hatuishi kwa kuogopa gharama za kilo/ mzani wa vitu, tunafuga na kutafuta Mali kwa juhudi zetu. Inawauma Nini? Kazi zilizowashinda wengi tunazifanya nalo tatizo?

Sisi hatuna mavitambi ya mafuta ya transfoma na broiler wa chanjo, tunakula vya kienyeji.
 
Chooni huwa unafuatilia.
Binafsi mimi ni Msukuma, kwa miaka 15 liyopita nimehamia Uchagani huku. Na niko huku nakula kama niliyokua nakula nyumbani. Tunatwanga ugali maziwa, na mboga za kutosha.

SIna overweight km wanaokula kidogo.Huku wanawache wanavutambi ila usukukumani hakuna mwanamke mwenye kitambi.
We haupo uchagani, upo upareni, ole wako uje huku uchagani ule kama vita, tutakumaliza!
 
Back
Top Bottom