HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Naomba kuuliza TAMISEMI wanahusika na vibali gani vya uhamisho na UTUMISHI wanahusika na vibali gani ?
 

Sahihi. Lakini tujue kuwa mwenye uamuzi wa mwisho wa kuamua ni KM Utumishi. Nimeshakutana na kesi boss aliandika negative na bado KM, kwa maslahi mapana ya utumishi akaamua uhame. Hiyo shortage kwanza unadhani KM Utumishi haijui? Asili ya maboss hata akiwa na watumishi wengi bado tu anatamani wajazane. Unakuta umekaa kituo fulani kwa miaka minne ukiwa peke yako. Baadae wanaongezeka wengine wawili mnakua watatu. Ukiomba kuhama, unaambiwa tuna shortage. Na miaka yote umefanya kazi na kila kitu kikaenda. Waajiri wawe na utu aisee kama mtu amepata nafasi huko anakoenda mruhusu tu aende tu hii ni kazi ya serikali haiwezekani mtu mmoja akiondoka taasisi yako itasimama.​
 
Naomba kuuliza TAMISEMI wanahusika na vibali gani vya uhamisho na UTUMISHI wanahusika na vibali gani ?

Utumishi - Kutoka taasisi moja kwenda nyingine/wizara moja kwenda wizara moja kwenda nyingine/halmashauri kwenda wizarani/wizarani kwenda halmashauri/halmashauri kwenda taasisi/taasisi kwenda halmashauri

TAMISEMI - Kutoka halmashauri moja kwenda nyingine

RAS - Kutoka halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya mkoa wake

DED - Kutoka work station moja kwenda nyingine ndani ya halmashauri yake
 
Asante nashukuru
 
Kabisa ila Rejection is direction
 
Jamani mimi mwenzenu Mwl Elimu msingi nilituma maombi ya uhamisho wa kubadilishana vituo vya Kazi na mtumishi mwenzangu kutoka halmashauri ya mkoa A kwenda halmashauri nyingine ya mkoa B. Kufikia mwezi September Mosi maombi yetu yalikuwa yamefika PO RALG TAMISEMI
Naombeni kujua tutegemee majibu ya vibali mwezi gani?
 
SEPTEMBER MOSI 2027
 
Mnielimishe mimi sipo kwenye mfumo rasmi wa ajira!
TAMISEMI ni nini? Kada zipi zipo chini yake?
UTUMISHI ni nini? Kada zipi zipo chini yake?
Kuna maneno yamerudiwa sana humu mfano wizara, mamlaka, taasisi n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…