Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Kumbe Mzee we ni empty set namna hii..
Uliwahi kuona wapi Nyerere amewekeza kwenye Elimu zaidi ya zile zile za wakoloni?

Aliona ni Bora kutumia pesa za Nchi kwenda kuanzisha vita ya Idd Amin kumsaidia Jamaa yake Obote.

Aliona Bora msalie wajinga ila atymie pesa za Umma ma Rasilimali watu nk kusambaza wanajeshi nk kupigana kwenye Nchi zingine.

Kimsingi hana lolote la maana Aliwahi fanya kwenye mambo ya Maendeleo zaidi ya kukandamiza Wapinzani wake na kuwapoteza.
 
Siyo makusudi bali ni kwa bahati mbaya au niseme kwa kutowajibika. Tatizo la watanzania ni elimu. Pengine utauliza mbona tuna vyuo na sekondari nyingi tu na idadi ya wahitimu ni kubwa? Jibu ni elimu yetu haifanyi watu waelimike bali kukariri kwa ujanja ujanja ili wapate vyeti. Ndiyo maana siku hizi unaona watu wanashindana kuonyesha kuwa ni wasomi kwa kutumia titles kama injinia, wakili msomi, Dr, CPA nk kabla ya kuandika majina yao. Hii ni inferiotity complex inayotokana na ''wasomi'' wengi kujiona hawana uwezo wa kushindana na wasomi wengine duniani hivyo wanajaribu kujiliwaza. Kukosa elimu sahihi kunafanya watu wasione correlation kati ya maisha yao na uongozi wa kisiasa na kukata tamaa mapema.
Mifumo ya ccm ndo imewafikisha WaTanganyika hapo.
Hadi Rais kila analazimisha aitwe Dr. Inferiority complex of the highest order.
 
kweli kabisa kwani yeye ndiye wa kwanza kukataa vyama vingi na kuleta udikteta wa chama kimoja, failed theories of villagisation, nationalisation and party supremacy. Na hata kipindi cha watu kuanza kuamka alikuwa akisema TV na friji ni luxuries ambazo watanzania hawahitaji (lakini yeye alikuwa na satellite dishes mbili kwake ikulu)
Nyerere alikuwa na Imani na sera zake. Hazikufanukiwa... Je, waliofuata walikuja na sera zipi?
 
1. Kutokutimiza majukumu (kulea, kufanya kazi, kujituma-uvivu, kushindwa kujisimamia n.k)

2. Miji michafu watu wanatupa taka ovyo wanataka mpaka wawekewe Sheria Kali ndiyo wafanye usafi mpaka kwenye majumba yao wenyewe.

3. Uzalendo hakuna kwenye Kila sekta.

4. Watanzania tuna matatizo/shida nyingi Sana sitaweza kuziandika zote Mkuu.
nikweli kabisa mkuu.lakini naona tumerisi kwa babu zetu walikuwa malofa sana sisi tunaendeleza tuu.

hatupendi kujifunza vitu vipya kabisa tunakalia ukale
 
Wewe ni mzalendo? Au Uzalendo wako ni kuja na kuwasimanga watanzania wenzako? Watu wajinga kama wewe ni rahisi mno kusaliti nchi zenu. Uzi wako unaashiria wewe ni kibaraka.
Mkuu ningekuona unajielewa kama ungejibu hiyo mifano yote niliyo kupa hapo juu.

Lakini fine naona hauna uwezo wakudiscuss our country issues na Mimi.

Naona hauna positive mind katika inchi yako, Mtu kuusema ukweli et ni kibaraka. Wewe naona ndiyo kibaraka cuz hautaki kuiponya jamii yako Kwa kuusema ukweli badala yake unasema ni masimango negative negative mindset.

At least ungejibu Kwa hoja hiyo mifano yangu niliyo kupa hapo juu lakini wewe naona unadank dank as mokey and you have nothing to tell me yani hauna hoja.

Naona kuusema ukweli tulionao Watanzania kwako kumekuwa ukibaraka.

Hauna hoja zaidi umejawa na negative negative mindset.
 
Ukitazama ujinga tulionao Watanzania wengi katika karne hii utagundua kuwa Mwalimu Nyerere alipambana sana.

Hakika Baba wataifa alipata tabu sana kusugua kutu na Msasa kwenye vichwa vya Watanzania.

Imagine ujinga wakipindi chake ulikuwaje kama hivi sasa ni 2025 Watanzania karibia wote tunaujinga mkubwa namna hii, Yani kuanzia ngazi za(familia) na kila kona ni ujinga ujinga, umbea umbea tu Lord have Mercy.
Nyerere hakua mutu alietaka watu wa elimike kwanza hakua anapatana na watu wenye elimu.wao Ndio wali fanya Elimu tusiipate
 
Acheni ujinga
Waulize waliosoma enzi zile za 60 na sabini. Elimu bure std one hadi PhD!! Usibishe kama wewe ni GenZ.
Wakoloni hawakujenga chuo kikuu. Ni JKN alijenga
Mkuu achana na hawa vijana wajinga wajinga ambao hata historia ya nchi yao hawaijui, Bali wameaminishwa ujinga ujinga na wazee wao wajinga nawao wakaamini ujinga huo so sad.
 
Yeye pia anacho Cha kulaumiwa kwa sera zake mbovu na siasa za ndio mzee ndo zilizotufikisha hapa kwahiyo na yeye hakwepeki kulaumiwa
 
Nyerere hakuelekeza kiswahili kitumike mashuleni alielekeza iwe lugha ya taifa. Ila English ni lugha ya kitaaluma na imekuwa hivyo miaka yote.

Ni miaka hii ndio hawa viongozi wa sasa wameanza kusema kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia.

Nyerere hakuwahi kusema kiswahili kiwe lugha ya kufundishia kitaaluma, wapi alisema hayo maagizo mzee?

Sasa kwa nyakati zile angesema watu wanaotakiwa kuwa wabunge waanzie degree, nani angepita mzee?😂😂😂 Hilo bunge si lingekuwa na watu kumi tu sababu ya wasomi kuwa wachache na hata waliosoma kutia nia ilikuwa mziki.

MIaka ile kwanza watu walikuwa wanaogopa uongozi kama kitu gani sijui hawakuwa na shobo hata kidogo. Mtu kuwa kiongozi ni hadi watu wamfosi ndio anaenda. Sio kama siku hizi watu wanahonga ili wawe wabunge.

Tu
Mkuu vijana wengi hawajui historia ya nchi yao wanamzushi hayati Baba wa Taifa maneno ya umbea umbea tu.

Wanasahau kipindi hicho kiswahili chenyewe watu walikuwa hawawezi watu wengi walikuwa wanaongea lugha za makabila yao.
 
Toa ujinga hapa,Elimu ya pyramid kama ya Mkoloni ndio unasema?

Wilaya nzima Ina sekondari Moja Hadi miaka ya JK ndio zinajengwa harafu unaleta nonsense zako hapa.
Mkuu tatizo umetanguliza lawama mbele so imekupiga Upofu kwenye mindset zako.

Nyerere alikuwa anamambo mengi Sana yakupambana nayo baada ya kushika madaraka asingeweza kufanya mambo yote, Ndiyo maana kuna awamu za kuongoza nchi.
 
Experiments za ujamaa za huyo huyo Nyerere ndio ziliwaponza mkawa hivyo, na itachukua miongo kadhaa kuja kuendana na dunia ya kisasa.
Mkuu ukisema hivyo Dunia itakushangaa eti unamtupia lawama hayati Baba wa Taifa kwasababu ya sera zake za ujamaa.

Nchi ngapi zilikuwa za kijamaa na leo wanamaendeleo?

Vipi Nyerere ametuzuia kufanya mabadiliko?

Tukisha mtupia lawama hayati enhee what next??

Mkuu lawama kwa marehemu zitasaidia nini?

Tumeshaelewa tatizo bado tumelikumbatia sisi na marehemu nani marehemu ?
 
Shule za sekondari zimeanza Kujengwa miaka ya Mkapa,JK, Mwendazake na Samia.

Miaka zaidi ya 35(25) ya Nyerere hakuna Cha maana anafanya zaidi y kuua Watoto wa watu kwenye mabita yasiyo na Msaada Kwa Nchi.

Kiufupi hakuwa na akili ndio maana mlikuwa mnamtukuza na alitaka muwe mbumbumbu Ili awatawale vizuri.
Aise so sadness Sana Kwa mindset hizi kazi ipo.
 
Yaani ujinga wa enzi za nyerere ni sawa na wa sasa??
Sasa kuna uoga ila sio ujinga.
 
Miaka 25 hakuna shule alijenga zaidi ya Wakoloni.

Mtu wa hivyo alikuwa na Msaada gani Kwa Nchi? Harafu mliojazwa ujinga mnamtukuza.

Kutwa kucha ni propaganda za kumsifu 🤣🤣
Hatumtukuzi Mkuu ila ni ukweli usiopingika kuwa hayati Baba wa Taifa ni kiongozi bora kuwahi kutokea.

Finally wewe naona ndiyo umejaza ujinga kichwani kwako kumuhusu mzee.
 
Back
Top Bottom