Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
- Thread starter
- #181
Government may be defined as an institution of the state that is primarily concerned with governance and the general well-being of the people within it’s governance.
Mimi sikumaliza Chuo UDSM, Mkuu labda nimekosea definition unaweza ukanisahihisha hapo.
Wala haujakosea hiyo ni maana ya serikali
Sasa kwenye serikali Kuna mgawanyo wa madaraka/mamlaka (separation of powers) na hapo ndipo ilipozuka mihimili mitatu ya serikali hasa katika mgawanyo wa mamlaka katika kuendesha serikali.
Mihimili hiyo ndio hushirikiana kuongoza Taifa na Serikali. Kumaanisha lengo linakuwa Moja
Ila Kila kimoja kinakuwa na mipaka yake.
a) Bunge (Parliament) Kutunga Sheria na kuisimamia serikali Kuu.
b) Mahakama (judiciary) kutoa Haki, kutafsiri Sheria
c) Serikali kuu (Executive) Kutekeleza Sheria na sera
Alafu hii mihimili ya Serikali ni katika nchi zinazotumia Demokrasia. Hivyo usije ukakariri Tena ukasema mihimili ya Serikali ni mitatu. Sema serikali za kidemokrasia.
Tukirudi kwenye dhana Yako ya mihimili ya Nchi.
Nchi Ili iitwe nchi lazima iwe na Watu, Ardhi, Utawala, utamaduni n.k.
Hakuna nchi isiyo na watu, Ardhi, utawala au utamaduni