Watu hawataki kutembeleana siku hizi, kila mmoja yuko bize kusaka shilingi

Na hili ndilo tatizo kubwa; Unafikiri ni nini kifanyike ili ile hali ya watu kuishi kiutu na kutembeleana iweze kurudi?
Mishahara iongezwe na ajira ziongezeke. Sikuhizi kazi watu wanafanyishwa kazi hadi Jumamosi nikiwamo mimi binafsi. Mapumziko yanakuwa Jpili tu.

Huo muda wa JPili huwezi acha kulala ukamtembelee mtu. Ni ngumu aheri zamani ilikuwa inaeleweka jmosi ni mapumziko na Jpili ni visiting day kwa ndugu jamaa na marafiki.
 
Tatizo hata ukiwa na hela huwezi kutembelea kila ndugu sababu wapo wanao hustle daily. Mtu ratiba yake anashinda sokoni ukitaka kumuona labda umtembelee sokoni.
 
Kujuana juana ndio kunaleta wivu na ushirikina miongoni mwetu waafrika upo sahihi kabisa. Ni mimi na familia yangu tu kwa sasa sipendi mazoea ya kiduwanze.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣. Kwamba tayari ushadhibitiwa na mkono wa nyani. Huo umbeya ndio siupendagi yani.
 
Kitu kipi kilichosababisha uadui uongezeke? Je maisha ya unayoishi sasa yanakupa furaha?
Hasidi Hana sababu
Mtu anaweza kukuchukia tu bila hata sababu za msingi....hata hujui anataka nini kutoka kwako ila tu ndyo kashakuwa adui yako
Maisha ninayoishi nayafurahia kwasababu furaha yangu siittegemei itoke kwa mtu yeyote
 
Hakika mkuu. Kwa sasa hata vijana walio single ni wengi kuliko walio kwenye mahusiano. Wengi wana hook up then maisha yanaendelea
Mfumo huu wa maisha ulikuwa states (Marekani) lakini slowly unaenea ulimwenguni.
Ngono imeuwa rahisi sababu inathaminishwa na hela,hata haya mahusiano ambayo baadhi yetu tunayo yameshikiliwa na fedha.

Unacho kiongea kinashamili kwa kasi sana na ndio maana siku hizi single mother ni wengi sana na watu hawataki kuwajibika.
 
Zamani waliwezaje, mishahara ilikuwa ni mikubwa? Miaka ya nyuma wengi walikuwa wakiishi katika mazingira ya kilimo na ufugaji pamoja na ujira mdogo, na walikuwa wakiishi kwa furaha zaidi, ila nyakati hizi za kutafuta hela bila kwenda shambani au ufugaji, ndio mienendo ya kijamii imebadilika, kwa nini iwe hivyo?
 
Mfumo wa sasa sababu ajira hamna watu wanajitafuta tu. Mtu unajua usipoenda ku hustle hutoboi so muda wa kukaa na kuwaza ndugu sijui kutembeleana unakuwa hakuna.
Nadhani kama tukirudi kwenye ufugaji na ukulima na kupelekea matumizi madogo ya fedha, kunaweza kurejesha ile hali ya zamani; hii unaionaje? Ila hii ya kutafuta mpaka ela ya kitunguu, lazima tuwe watumwa.
 
Kujuana juana ndio kunaleta wivu na ushirikina miongoni mwetu waafrika upo sahihi kabisa. Ni mimi na familia yangu tu kwa sasa sipendi mazoea ya kiduwanze.
Ukiwa mgonjwa utatamani utembelewe na jamii ya watu wengi, vinginevyo watakuja wawili tu.
 
Zamani ukipewa laki we huimalizi mwezi mzima na unafanya anasa zote. Leo hii laki kumaliza week ni kipengele 🤣
 
Hasidi Hana sababu
Mtu anaweza kukuchukia tu bila hata sababu za msingi....hata hujui anataka nini kutoka kwako ila tu ndyo kashakuwa adui yako
Maisha ninayoishi nayafurahia kwasababu furaha yangu siittegemei itoke kwa mtu yeyote
Huo ubinafsi, utakupa furaha pale utakapokuwa umelazwa hospitali na ukatembelewa na mtu mmoja tu?
 
Zamani ukipewa laki we huimalizi mwezi mzima na unafanya anasa zote. Leo hii laki kumaliza week ni kipengele 🤣
Nilichogundua, chanzo cha matatizo haya yote, ni kwa sababu hatuzalishi; wote tunagombania vitu vilivyozalishwa na watu wachache (wakulima, viwandani); na hii kupelekea kuwa watumwa kwenye kusaka hela, badala ya kuwa watumwa kwenye kuzalisha vitu(mazao, au vitu vya kuuza).​
 
Ngono imeuwa rahisi sababu inathaminishwa na hela,hata haya mahusiano ambayo baadhi yetu tunayo yameshikiliwa na fedha.

Unacho kiongea kinashamili kwa kasi sana na ndio maana siku hizi single mother ni wengi sana na watu hawataki kuwajibika.
Hawazalishi chochote, kwa hiyo ili apate hela ya kununua mihogo inabidi aangalie ni nini cha kuuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…